WAZIRI PINDI CHANA AZINDUA MAFUNZO YA MAAFISA 700 UHAMIAJI ATAKA WADAU KUCHEZA NA PASI YA MAMA SAMIA SULUHU HASSAN |Shamteeblog.

Afisa Mtendaji Mkuu Chuo  Cha Taifa Cha Utalii Dkt.Shogo Mlozi akizungumza kwenye uzinduzi  huo.
Kamishna Generali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala
Maafisa wa Uhamiaji wakifuatilia uzinduzi huo.

Na Khadija Kalili
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Balozi Dkt.Pindi Chana amezindua Programu ya uimarishaji huduma kwa kupitia mafunzo kwa wadau walioko katika mnyororo wa huduma za Utalii nchini ambapo kwa kuanzia Maofisa 700 wa Idara ya Uhamiaji watapata fursa ya kujengewa uwezo katika Chuo Cha Taifa Cha Utalii kilichopo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo Agosti 20,2022 katika Chuo Cha Utalii na kushuhudiwa na jopo la Maofisa Uhamiaji, wadau wa Utalii, Dkt. Pindi Chana ametoa pongezi kwa Uongozi wa Chuo hicho kupitia kwa Mkurugenzi wake Dkt. Sholo Mlozi na bodi yote kwa kufikiria kutoa fursa hiyo adhimu ya mafunzo ya Utalii kwa watu wa kada mbalimbali huku akiunga mkono Kauli Mbiu ya Chuo hiko isemayo 'Cheza na Pasi ya Mama'.

"Kama mnavyofahamu hivi karibuni Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan alizindua filamu ya Royal Tour ambayo imefanikiwa kuwa na mvuto duniani kote na nakiri kwa kusema kuwa imetuletea watalii wengi na wapi ambao wamekuwa wakija zaidi ya mara moja kutembelea vivutio vyetu" alisema Mheshimiwa Balozi Dkt. Pindi Chana.

Idara ya Uhamiaji wako katika kila eneo la nchi ambako kote huko hukutana na watalii kwa njia moja au nyingine hivyo nawatakia masomo mema na mkazingatie yote ili kuboresha zaidi namna ya utoaji huduma" alisema Dkt. Chana.

Kamishna Generali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala amesema kuwa kwa niaba ya Uhamiaji amemshukuru kwa fursa waliyopatiwa Maofisa wake na kupewa kipumbele cha kupatiwa mafunzo hayo huku akiahidi kuwa yatazaa matunda yenye tija kwa upande wa Idara yao na Taifa kwa ujumla.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Utalii Dkt. Shogo Mlozi amesema kuwa Utalii ni uzoefu ambao mgeni anaupata kwenye husika ama sehemu anayoitembelea hivyo katika kupata uzoefu huo wa Utalii wadau mbalimbali wanahusika katika kutoa huduma ndipo wakaona kuna umuhimu wa kutoa mafunzo kwa fani mbalimbali ikiwa ni pamoja na Waandishi wa Habari.

"Maafisa Uhamiaji hukutana na wageni wengi na wenye mahitaji mbalimbali wanaotoka na kuingia nchini kwa shughuli tofauti ikiwemo Utalii ,hivyo Ili kuongeza idadi ya watalii nchini ni lazima kujenga mahusiano mazuri baina ya sekta ya Utalii hivyo shughuli za Ulinzi na Usalama ni eneo muhimu sana kwa ustawi wa Utalii" alisema Dkt. Shogo

Aidha ifahamike kwamba mafunzo haya ni muendelezo wa jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na serikali,wadau pamoja na viongozi wetu hasa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuinua sekta ya Utalii na kuifanya kuwa stahmilivu zaidi baada ya kudorora kwa huduma kutokana na na janga la UVIKO-19.

Aidha Dkt. Shogo amesema kuwa Chuo hicho kinatembea na Kaulimbiu isemayo "Cheza na Pasi ya Mama' ikimaanisha kuwa Rais Mama Samia amepiga pasi hivyo wadau ambao wako katika mnyororo wa huduma za Utalii wafunge magoli.

Mafunzo hayo ya Maofisa Uhamiaji yamedhamini na Benki ya NMB kwa udhamini wa Mil.20.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post