Dier: Wazimu wa mashabiki wa mechi za ugenini unatisha |Shamteeblog.

Siku zote kucheza mechi mbali na kiwanja ulichokizoea kunaleta wasiwasi.

Hii sio tu kwa mashabiki, bali hata wachezaji. Sikia hii.

Beki wa Tottenham Hotspur Eric Dier anasema tabia za mashabiki wa mechi za ugenini siku zote zina wazimu ambao wakati mwingine huwapelekea kufanya vurugu.

Na hili limekuwa tatizo kubwa sana katika viwanja vingi na ndio maana hajisijkii furaha kwa familia yake kwenda kumuangalia yeye anapocheza katika viwanja vya ugenini kwa sababu hiyo.

Kauli yake inakuja baada ya usalama wa mashabiki wanaokuwa ugenini kuonekana kuwa mashakani kwa mashabiki wageni.

Ligi ya Uingereza ( EPL) hivi karibuni ilisema kuwa itachukua hatua ya kuwalinda mashabiki wanaosafiri kwenda katika viwanja vingine visivyo vya timu zao kwa sababu ya tabia hatarishi za mashabiki wenyeji.

EPL imeongeza kuwa timu zisizo wenyeji zitapewa ulinzi wa kutosha zinapokuwa ugenini.

Dier anasema baadhi ya ndugu na marafiki zake walipata matatizo wakati klabu yake ilipokuwa ugenini Standford Bridge na kutoka sare ya 2-2 na Chelsea.

” Walipata tabu sana jamaa zangu”,

” Siwezi kusema wenye tabia ya vurugu ni mashabiki wa Chelsea tu , bali ni wa timu yoyote wanapokuwa wenyeji,” amesema.

Mwaka 2020, Dier alifungiwa mechi 4 na FA ya Uingereza kwa kosa la kufokeana na shabiki baada ya timu yake kufungwa na Norwich City.

” Hii inaogopesha na ndio maana familia yangu haiendi katika mechi za ugenini sababu ya vurugu za wenyeji,” amesema.

The post Dier: Wazimu wa mashabiki wa mechi za ugenini unatisha appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post