Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azzan Zungu ameitaka wizara ya Fedha na Mipango kuongeza usimamizi wa ukusanyajji wa mapato ya Serikali ambayo ameeleza kuwa hayaridhishi.
Amesema ukiangalia mapato ya bandari na yale yanayokusanywa katika bandari nyingine za kigeni hayalingani kwa sababu ya ukusanyaji hafifu.
” Kwa mfano makusanyo ya bandari yetu kwa mwezi ni bilioni 95 wakati katika bandari za nchi jirani makusanyo yanafika mpaka bilioni 300 kwa mwezi.”amesema.
Pia amemtaka Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Nnauye, kuona namna watakavyoweza kushirikiana na Wizara ya Fedha, kuja na mfumo thabiti utakachochea ongezeko la mapato ya serikali kupitia matumizi ya data.
The post Zungu aitaka serikali kukusanya mapato ipasavyo appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment