Israel kuiuzia UAE teknolojia ya kujilinda na mashambulizi ya anga |Shamteeblog.

Israel itaiuzia Umoja wa nchi za Falme za Kiarabu ( UAE) teknolojia itakayoiwezesha kujilinda na mashambulizi yanayofanywa na ndege zisizo na rubani ( Drones).

Ukiachilia mbali biashara, mauzo hayo pia yana lengo la kukuza uhusiano baina ya pande hizo mbili, imeelezwa.

Shirika la habari la Uingereza, Reuters limethibitisha kuwa Israel tayari imepitisha mauzo hayo.

Chanzo kingine cha habari kimesema UAE inaitaka Israel iiuzie teknolojia ya kupambana na mashambulizi ya anga yanayofanywa na drone ili isishambuliwe kama ilivyoshambuliwa Abu Dhabi hivi karibuni.

Ram Ben Barak, Waziri wa Israel anayehusika na Mambo ya Nje aliulizwa hivi karibuni kuhusu mpango huo, lakini alikataa kusema chochote kuhusiana na biashara hiyo.

Na badala yake alisema kuna mahusiano baina ya pande hizo mbili.

UAE imekuwa ikishambuliwa kwa roketi na drone na kundi la waasi linalojulikana kama Housi la nchini Yemen.

Mpango huo unakuja wakati ambao Marekani na Israel zinatoa msukumo kwa mataifa ya Kiarabu kutengeneza mfumo wa kujilinda dhidi ya Iran.

Hata hivyo, mpango huo umepingwa na mataifa ya kiarabu na haujatekelezwa mpaka sasa.

The post Israel kuiuzia UAE teknolojia ya kujilinda na mashambulizi ya anga appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post