CHIFU MWAKATUMBULA WA WANYAKYUSA AANZA KAZI RASMI |Shamteeblog.


Katika kutekeleza adhima ya Mhe Rais Samia Suluh Hassan  ambaye ni kiongozi wa machifu nchini Chifu 'Hangaya'  ya kuuhuisha kuendeleza tamaduni za kichifu nchini, Hatimaye Chifu wa kabila la Wanyakyusa ,Chifu Edwin Mwakatumbula leo amekabidhiwa Ikulu yake ya Kichifu na kiongozi wa machifu wadogo wa kabila hilo.

Akizungumza katika tukio hilo la kihistoria, Chief Edwin amesema kuwa imekuwa siku ya baraka kwenye himaya hiyo, kwa yeye kukabidhiwa Ikulu hiyo iliyojengwa Mwaka 1900 huku akiahidi kuendeleza umoja, mila na tamaduni za kabila hilo.

Amesema kuwa aliporithi uchifu wa kabila hilo kutoka kwa marehemu Chifu Daudi B Mwakatumbula miaka 10 iliyopita amejitahidi kuendeleza mila za kabila hizo huku akidumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wanyakyusa wote nchini.

Mbali ya kuwa Chifu, Edwin ana historia kubwa kwenye siasa za nchi hii, huku akihudumu kwenye nafasi mbalimbali za kiungozi na kiutawala kwenye maeneo mbalimbali nchini ambapo kwa nyakati tofauti amehudumu kama Katibu wa Chama cha Mapinduzi  ngazi ya wilaya ambapo mara ya mwisho alikuwa katibu wa chama wilaya ya Geita.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post