NA YEREMIAS NGERANGERA…..NAMTUMBO.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Dkt Julius Kenneth Ningu amewataka wazee na wananchi wa wilaya ya Namtumbo kutumia fursa iliyotolewa na Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kujiandikisha ili waweze kunufaika na fursa ya kununua mbolea iliyowekewa Ruzuku ya serikali.
Dkt Ningu aliyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee wilayani humo ambapo aliwataka wazee kutumia fursa iliyotolewa na serikali ya kujiandikisha ili waweze kunufaika na fursa iliyotolewa na serikali ya kuwawezesha kununua mbolea iliyowekewa ruzuku .
Aidha Dkt Ningu aliwaambia wazee wa wilaya ya Namtumbo kuwa malalamiko makubwa ya wakulima wa wilaya ya Namtumbo ilikuwa ni bei kubwa ya mbolea ,hivyo serikali imesikiliza kilio hicho na kuamua kutoa ruzuku kwenye mbolea ili kupunguza bei ya mbolea kwa wakulima.
Hata hivyo Dkt Ningu aliwaambia wazee hao kuwa ili waweze kunufaika na fursa ya kununua mbolea iliyowekewa Ruzuku ya serikali ni lazima kujiandikisha na kujipatia namba ya mkulima na kinyume cha hapo hawataweza kunufaika na fursa hiyo ya serikali na kudai kuwa kujiandikisha ni bure .
Rajabu Karumbeta pamoja na kuipongeza serikali kwa kuwajali wazee alimwomba mkuu wa wilaya kushughulikia changamoto ya upatikanaji wa dawa katika zahanati licha ya kuwepo dirisha maalumu kwa ajili ya wazee lakini changamoto ya upatikanaji wa dawa ni tatizo kwa wazee kwani inawapa wakati mgumu kununua dawa katika maduka ya dawa huku maisha yao wanashindwa kumudu kugharimia kununua dawa hizo alisema Tarumbeta
Tarumbeta alitumia nafasi hiyo pia kuwasilisha maombi yao kwa serikali ya kulipwa pesheni ya wazee ili waweze kufurahia maisha yao ,kwa kuwa wazee hao wametumia akili na nguvu zao katika kulijenga taifa hili alisema Tarumbeta.
Daktari Aisha Makange aliwataka wazee kuzingatia lishe bora ili kuepukana na magonjwa yanayotokana na kutozingatia ulaji wa vyakula akitolea mfano wa unywaji wa vinywaji mfululizo kama enegy,pespsi na vinywaji vinginevyo huleta madhara kiafya alisema Makange.
Makange alisema ipo homa ya kisukari , shinikizo la damu (bp) inayosababishwa na kutozingatia matumizi sahihi ya vyakula tunavyokula na kuwataka wazee hao kuzingatia lishe ili kujinusuru na madhara yatokanayo na kutozingatia lishe bora . Wazee wa wilaya ya Namtumbo wameungana na wezee wenzao duniani kuazimisha siku ya wazee ambapo huazimishwa kila mwaka tarehe 1 mwezi wa kumi na kauli mbiu ya siku ya wazee duniani kwa mwaka huu 2022 ni “Ustahimilivu na mchango wa wazee ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa”
By Mpekuzi
Post a Comment