Jurgen Klopp anasema Liverpool haitakiwi kutabirika katika mfumo wake wa uchezaji ili kurejea katika ubora wake wa msimu uliopita.
Liverpool wanajiandaa kwa ajili ya mchezo wao Jumapili dhidi ya Arsenal wakiwa wameshinda mara mbili pekee katika mechi tano zilizopita, wakiwa na ‘clean sheet’ ya mechi mbili pekee katika mechi tisa za Premier League walizocheza hadi sasa.
Kusuasua kwao katika msimu huu kumewafanya wawe nyuma kwa pointi 11 dhidi ya Arsenal ‘ The Gunners’ ambao ndio wanaongoza ligi kwa sasa.
Klopp anasema kuamua kwa Liverpool kutumia mfumo wa 4-4-2 na kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Rangers katika Ligi ya Mabingwa katikati ya wiki kumekuwa na matokeo mazuri.
“Ni muhimu kutotabirika tena,” alisema klopp kabla ya safari ya kuifuata Arsenal Emirates. “Tunahitaji mifumo tofauti, kwa hivyo inabidi timu pinzani zijue kuwa [4-3-3] sio mfumo pekee tunaoweza kucheza.
“Unapoona tatizo na kulifanyia utatuzi ndio pekee ya kurudi katika ubora,”. “Tunaendelea kutafuta ufumbuzi kwa matatizo yetu ili tuwe bora zaidi,”amesema.
The post Klopp: Mfumo wetu wa uchezaji hautabiriki appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment