Zaidi ya nchi 40 za Jumuiya ya Ulaya zinakutana mjini Prague katika mkutano wa kujadili amani inayodaiwa kuvurugwa na Urusi kwa kuivamia Ukraine.
Akiwasili kwa ajili ya mkutano huo, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema mkutano huo unalenga kujadili vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine .
Waziri Mkuu wa Uingereza Liz Truss alikutana na viongozi kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Uturuki na Norway kujadili vita inayoendelea kati ya mataifa hayo mawili barani humo.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelesky pia ameshiriki mkutano huo kwa njia ya video.
Mkutano huo wenye kuunganisha jumuiya ya nchi za Ulaya kwa kiasi kikubwa umeandaliwa na na Rais wa Ufaransa.
Viongozi hao pia wamejadili suala la upatikanaji wa nishati , usalama pamoja na ukimbizi , huku vita ya Urusi- Ukraine ikiwa ajenda kuu.
The post Urusi yaipasua kichwa Jumuiya ya Ulaya appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment