MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI YATOA MCHANGO WA VITABU NA KEMIKALI KWA WILAYA YA HANDENI |Shamteeblog.

Mkuu wa wilaya ya Handeni, Mhe. Siriel Mchembe (aliyesimama), akihutubia katika hafla ya kupokea vitabu vya masomo ya sayansi nakala 786 kwa kidato cha tano na sita na kemikali za maabara kwa ajili ya masomo kwa vitendo. Mchango huo umetolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), kama juhudi za kuiunga mkono Serikali katika kuhamasisha wanafunzi kusoma na kupenda masomo ya sayansi. Katika picha, wa pili kutoka kulia ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi, Evaclotida Kapinga (kulia) na Meneja wa Kanda ya Kaskazini, Arusha, Christopher Anyango (kushoto). Hafla hiyo imefanyika katika Shule ya Sekondari Mkata, Oktoba 18, 2022.

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama), akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi katika hafla ya kikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi na kemikali za maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi kwa vitendo kwa wanafunzi wa shule za sekondari za wilaya ya Handeni. Vitabuna kemikali hizo zimekabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya ya Handeni.
Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi (GCLA), Evaclotida Kapinga (aliyesimama), akiwasisitizia jambo wanafunzi kuhusu umuhimu wa kusoma na kupenda masomo ya sayansi pamoja na kuwahimiza walimu kuendelea kutoa mchango wa elimu bora katika masomo ya sayansi.
Picha ya juu: Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkata wakisikiliza hotuba kutoka kwa viongozi mbalimbali wakati wa hafla ya kupokea vitabu vya masomo ya sayansi nakala 786 na kemikali za maabara kwa ajili ya masomo kwa vitendo.
Picha ya chini: Baadhi ya wazazi na walimu wakiwa katika hafla.
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Mhe. Siriel Mchembe (aliyevaa koti la bluu bahari)), akikata utepe wakati akipokea vitabu vya masomo ya sayansi na kemikali za maabara kwa ajili ya masomo kwa vitendo kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyevaa Kaunda suti) Katika picha kushoto na kulia ni wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkata.

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (katikati), akionesha aina ya vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, ambavyo ni vya masomo ya Baiolojia, Kemia, Hisabati na Fizikia kwa kidato cha tano na sita. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Siriel Mchembe na kulia ni Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kaskazini, Christopher Anyango.
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Handeni, Saitoti Stephen (wa pili kutoka kulia), akiwakabidhi vitabu walimu wa Shule ya Sekondari Mkata. Kushoto ni Afisa Elimu Sekondari Handeni, John Lupenza.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (watatu kutoka kushoto), akitoa maelekezo kwa Afisa Elimu Taaluma Handeni, Basil Mrutu (kulia), kuhusu matumizi salama ya kemikali zilizotolewa na Mamlaka kama ‘sulphuric acid’ alipotembelea maabara ya Shule ya Sekondari Mkata.
Mwanafunzi wa kidato cha nne, Shule ya Sekondari Mkata, Sophia Nasoro (wapili kutoka kulia) akionesha namna wanavyofanya mafunzo kwa vitendo kwenye maabara kwa wageni mbalimbali (hawapo pichani), walipo tembelea maabara ya shule hiyo. Kulia ni mwalimu wa somo la Kemia, Shule ya Sekondari Mkata.
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Mhe. Siriel Mchembe (katikati), Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa nne kutoka kulia) wakiwa pamoja na viongozi mbalimbali na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkata (walioshika vitabu) mara baada ya kukamilisha hafla ya kukabidhi vitabu na kemikali kwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni Oktoba 18, 2022.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post