LSF YAANDA MPANGO MKAKATI KUTATUA CHANGAMOTO ZA KISHERIA |Shamteeblog.

Muwakilishi wa Msajili wa Huduma za Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria nchini, Wakili Agness Mkawe akizungumza na watoa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau uliondaliwa na LSF pamoja na wadau wake nchini nzima kwa ajili ya kutathmini utekelezaji za programu ya upatikanaji wa haki nchini inayotekelezwa na LSF.
Meneja Programu wa Legal Services Facility (LSF), Wakili Deogratias Bwire akizungumza na watoa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau uliondaliwa na LSF pamoja na wadau wake nchini nzima kwa ajili ya kutathmini utekelezaji za programu ya upatikanaji wa haki nchini inayotekelezwa na LSF.
Muwakilishi wa Msajili wa Huduma za Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria nchini, Wakili Agness Mkawe akiwa kwenye picha ya pamoja na watoa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau uliondaliwa na LSF pamoja na wadau wake nchini nzima kwa ajili ya kutathmini utekelezaji za programu ya upatikanaji wa haki nchini inayotekelezwa na LSF.
Washiriki wa mkutano wakifuatilia mkutano wa wadau uliondaliwa na LSF pamoja na wadau wake nchini nzima kwa ajili ya kutathmini utekelezaji za programu ya upatikanaji wa haki nchini inayotekelezwa na LSF.


SHIRIKA lisilo la kiserikali linaloshughulika na masuala ya msaada wa kisheria nchini(LSF) kwa kushirikiana na wadau wa sekta hiyo zaidi ya 400,wamekutana kwa ajili ya kutathimini namna ya utekelezaji programu ya upatikanaji haki nchini kwa mwaka 2022/2023.

Akizungumzia mkutano huo,Meneja programu kutoka (LSF) Wakili Deogratius Bwire amesema wadau watajadili mafanikio,changamoto na mipango mikakati kwa ajili ya utekelezaji wa programu hiyo katika mwaka ujao.

Bwire amefafanua zaidi kuwa Mkutano huo utawezesha wadau wa (LSF) ambao ni mashirika nufaika wa programu hiyo, kutoa mrejesho wa utekelezaji wa shughuli za msaada wa kisheria,kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu mbalimbali kwa ajili ya kujijenga na kujiimarisha kwenye masuala yote yanayohusu huduma za msaada wa kisheria.

"Matumaini yangu kikao hiki kitajadili na kutoka na mapendekezo,mikakati ya utekelezaji ili kuongeza tija na kuboresha ubora wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria ili kupata matokeo chanya katika jamii."

Kwa upande wa Msajili wa Huduma za Msaada wa wakili wa Serikali, Agnes Mkawe ameipongeza (LSF) kwa kuandaa mkutano huo kwa kuwa unalenga kuleta ustawi kwenye sekta ya msaada wa kisheria.

"Ushirikiano huu undelee zaidi na zaidi katika kuhakikisha huduma ya msaada wa kisheria unatolewa unakuwa wenye tija na manufaa kwa umma wa watanzania".

Aidha ameeleza kuwa wana washukuru wadau wa Maendeleo kama shirika la Kimataifa kutoka nchini Denmark (DANIDA) kwa kuwezesha (LSF) ili waweze kutekeleza programu yao.

Mkawe amechukua hatua nyingine na kuyataka mashirika yanayotoa huduma za msaada wa kisheria kujisajiri katika mfumo wa kielektroniki ili yaweze kutambulika ambapo amesema kati ya mashirika 1,047 ,mashirika 220 ndiyo yaliyosajiri.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post