Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya imeahirishwa tena leo Jumatatu, Novemba 21, 2022 kwa sababu hakimu anayesimamia kesi hiyo ana majukumu mengine.
Upande wa mashitaka umeieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kuwa hakimu Salome Mshasha yupo kwenye majukumu mengine ya kikazi.
Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashitaka saba ikiwemo uhujumu uchumi.
Hata hivyo, wakati yeye akiwa mahabusu kwa zaidi ya siku 170, wenzake Sylivester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey waliachiwa baada ya kukiri kutenda makosa ya uhujumu uchumi.
Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Jenifa Edward alieleza upande wa mashitaka wameeleza hakimu anayesikiliza kesi hiyo yupo kwenye shughuli nyingine akaahirisha kesi hiyo mpaka Disemba 5, 2022.
The post Kesi ya Sabaya yaahirishwa appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment