Ronaldo aanza mazoezi Qatar kuivaa Ghana |Shamteeblog.

Ronaldo ameanza mazoezi akiwa na timu yake ya Ureno ikijiandaa na mechi yake dhidi ya Ghana hapo Jumatano.

Hii itakuwa michuano ya tano ya kombe la Dunia kwa mchezaji huyo kucheza.

Hata hivyo, huenda ikawa ndio michuano yake ya mwisho kwa sababu ya umri wake.

Hii ni kwa sababu aliwahi kugusia kustaafu kwake katika siku za nyuma.

Ronaldo, mwenye miaka 37, amejiunga na timu yake ya taifa kwa ajili ya michuano hiyo mikubwa.

Licha ya mgogoro na timu yake ya Manchester United, staa huyo anaonekana yupo sawa kimwili na kiakili kwa ajili ya kipute hicho.

Ureno ipo kundi H na inajiandaa na mchezo wake dhidi ya Ghana siku ya Alhamisi.

Baada ya hapo, watacheza na Uruguay Novemba 28 na Korea Kusini Desemba 2.

Mshambuliaji huyo amekuwa katika wakati mgumu na timu yake baada ya kufanya mahojiano na Piers Morgan wa Talk TV kuwa klabu hiyo imemsaliti.

Katika mahojiano hayo, pia amesema kuwa Manchester United imekuwa na mwenendo mbaya toka Sir Alex Ferguson alipoondoka.

Pia alizungumzia mahusiano yake mabaya na kocha wake Erick ten Hag.

The post Ronaldo aanza mazoezi Qatar kuivaa Ghana appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post