Livingston Lusinde "Bashiri Ally Aachie Nafasi Aliyoteuliwa na Rais" |Shamteeblog.


Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa ya Chama cha Mapinduzi Livingston Lusinde (Kibajaji) amemshauri aliyekuwa katibu Mkuu wa Chama hicho ambaye ni Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Dkt Bashiri Ally kuachia nafasi ya Ubunge kwani ametoa kauli za Uchochezi zinazodaiwa kuashiria kutokuwa na imani na Rais ambaye ndiye aliyemteua kuwa Mbunge.
Lusinde amesema hayo Jijini Dodoma kutokana na kauli alizotoa Dkt Bashiru zilizotafsiriwa kuleta utata wakati akizungumza katika Warsha ya kitaifa ya Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) Mkoani Morogoro.
Lusinde amesema wakati Dkt Bashiru akiwa katibu Mkuu wa CCM ndiye aliyeanzisha utaratibu wa kusifia sasa anashangaa kuona akikerwa na Serikali ya awamu ya 6 kusifiwa wakati yeye pia ni Mbunge wa Ikulu (wa Kuteuliwa).


from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post