Makatibu wa Wakuu wa Serikali za Mitaa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki watembelea DART |Shamteeblog.


Mkurugenzi wa Fedha na Maendeleo ya Biashara Deus Kasmir akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya Makatibu  Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Serikali za Mitaa wakati walipotembelea mradi wa Mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.
 

 

*DART yasema utoaji wa huduma washangaza baadhi ya nchi ya Afrika

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

WAKALA wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) umesema kuwa mradi wa mabasi yaendayo haraka umekuwa kivutio baadhi ya nchi ya Afrika kuja kujifunza na wengine kutaka nchi zao kuwa na uwekezaji huo.

Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Fedha na Maendeleo ya Biashara wa DART Deus Kasmir  kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa wakati DART walipotembelewa na Makatibu Wakuu wa Serikali za Mitaa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliofika kujionea huduma za usafiri wa Umma uendeshwa katika jiji la Dar es Salaam.

Kasmir amesema kuwa mradi wa mabasi yaendayo haraka  kwa sasa ndio unakuwa na unatembelewa na mataifa mbalimbali namna wanavyoweza kutoa huduma ya usafiri unaofanya kuchochea uchumi wa nchi kutokana wananchi kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Amesema kuwa wakati wakitembelea mifumo DART wanapata picha namna wanavyodhibiti fedha kupitia mifumo hiyo ambapo imeonesha Tanzania imepiga hatua kwenye mifumo ya kieletroniki kwa serikali kujua mapato yake.

Aidha amesema kuwa ziara ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameonesha baadhi ya nchi kuja kujifunza na kwenda kutekeleza nchini mwao katika kutoa huduma za usafiri wa Umma kwa wananchi.

Hata hivyo amesema kuwa licha ya kuwa kivutio wakala unaendelea kuboresha huduma za usafiri pamoja ba mifumo mbalimbali kutokana na teknolojia inabadilika kila siku.

"Mradi wa Mabasi umekuwa kivutio kazi yetu DART ni kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwani hicho ndio kipaumbele chetu na tunasimama kwenye hicho kipaumbele hicho"amesema Kasmir

Meneja wa Miundombinu wa DART Mhandisi Mohamed Kaganda akitoa maelezo kwa Makatibu Wakuu wa Serikali za Mitaa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Tanzania na kujifunza Huduma za Usafiri wa Umma unaotolewa na Wakala wa Mabasi Yaenday Haraka (DART,) jijinii Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Uratibu wa Sekta wa Ofisi ya Rais,Tawala za Serikali za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Enock Nyanda akikabidhi zawadi zilizotolewa na DART mara baada ya kutembelea mradi wa mabasi yaendayo haraka na miundombinu  yake kwa Makatibu Wakuu wa Serikali za Mitaa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Baadhi picha  za Makatibu wa Wakuu wa Serikali za Mitaa wa Jumuiya ya Afrika na Watendaji wa DART wakiwa katika Basi ambalo limetumika kuonyesha mradi wa DART unavyofanya kazi wakati makatibu wa wakuu hao walipotembelea mradi huo kuona na kujifunza jijini Dar es Salaam.
 


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post