Polisi walaani mauaji ya kiongozi wa kimila Nigeria |Shamteeblog.

Kiongozi wa kimila ameuawa pamoja na wasaidizi wake wawili nchini Nigeria katika mauaji ya kutatanisha akiwa nyumbani kwake.

Wauaji hao inasemekana walikwenda nyumbani kwa kiongozi huyo na kujifanya wamepata taarifa ya dharura , lakini baadae waliwafyatulia risasi.

Kwa mujibu wa mamlaka za Nigeria, wauaji hao pia walivamia ofisi ya kijiji na kuua mtu mmoja na kupora pikipiki tatu.

Polisi wanatilia shaka kuwa watu wa kikundi cha Biafran ndio wamehusika na mauaji hayo.

Hata hivyo, kikundi hicho hakijasema chochote mpaka sasa.

Kikundi hicho kinadaiwa kufanya uasi kwa ajili ya kushinikiza kugawanywa kwa mji wa Biafra.

Na mara nyingi kikundi hicho kimekuwa kikihusishwa na machafuko katika eneo hilo la Biafra ndani ya jimbo la Imo.

The post Polisi walaani mauaji ya kiongozi wa kimila Nigeria appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post