Mkurugenzi wa Sekta za Jamii Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dkt. Irene Isaka , akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la siku mbili la Maendeleo ya Teknolojia kupitia tafiti mbalimbali lililoandaliwa na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kwa kushirikiana na GIZ lililofanyika leo Novemba 24,2022 jijini Arusha.
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki,akizungumza na wafugaji wakati wa hafla ya kugawa madume bora 50 ya ng’ombe aina ya boran kwa Vikundi vya wafugaji katika wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma iliyofanyika leo Novemba 24,2022.
SEHEMU ya Wafugaji na Viongozi wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki,akizungumza wakati wa hafla ya kugawa Madume bora 50 ya ng’ombe aina ya boran kwa Vikundi vya wafugaji katika wilayani Chamwino Mkoani Dodoma hafla iliyofanyika leo Novemba 24,2022.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mhe. Gift Msuya,akizungumza wakati wa hafla ya kugawa Madume bora 50 ya ng’ombe aina ya boran kwa Vikundi vya wafugaji katika wilayani humo Mkoani Dodoma hafla iliyofanyika leo Novemba 24,2022.
Kaimu Katibu Mkuu Sekta ya Mifugo, Dkt. Asimwe Rwiguza,akitoa taarifa wakati wa hafla ya kugawa Madume bora 50 ya ng’ombe aina ya boran kwa Vikundi vya wafugaji katika wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma hafla iliyofanyika leo Novemba 24,2022.
Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko kutoka Sekta ya Mifugo, Bw. Stephen Michael,akielezea hali ya mifugo iliyopo nchini wakati wa hafla ya kugawa Madume bora 50 ya ng’ombe aina ya boran kwa Vikundi vya wafugaji katika wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma hafla iliyofanyika leo Novemba 24,2022.
MENEJA wa Taasisi ya PASS Trust kutoka Mwanza Bi.Langelika Kalebi,akizungumza wakati wa hafla ya kugawa Madume bora 50 ya ng’ombe aina ya boran kwa Vikundi vya wafugaji katika wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma hafla iliyofanyika leo Novemba 24,2022.
MWENYEKITI wa wafugaji Wilaya ya Chamwino, Bw. John Kochocho,akitoa neno la shukrani kwa Wizara ya Mifugo mara baada ya kukabidhi Madume ya Ng'ombe wakati wa hafla ya kugawa Madume bora 50 ya ng’ombe aina ya boran kwa Vikundi vya wafugaji katika wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma hafla iliyofanyika leo Novemba 24,2022.
MWENYEKITI wa Kikundi cha Wafugaji Chamwino Bw.Mailosi Malogo,akiishukuru Serikali kwa kuwagawia Madume ya Ng'ombe wakati wa hafla ya kugawa Madume bora 50 ya ng’ombe aina ya boran kwa Vikundi vya wafugaji katika wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma hafla iliyofanyika leo Novemba 24,2022.
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki,akigawa Madume 50 Kwa Vikundi vya wafugaji Chamwino wakati wa hafla ya kugawa madume bora 50 ya ng’ombe aina ya boran kwa Vikundi vya wafugaji katika wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma iliyofanyika leo Novemba 24,2022.
MUONEKANO wa Madume 50 yaliyokabidhiwa kwa Vikundi vya wafugaji wa Chamwino leo Novemba 24,2022.
....................................
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amesema ugawaji wa madume ya bora ya ng’ombe ni utekelezaji wa mpango wa mabadiliko wa Sekta ya Mifugo.
Waziri Ndaki ameyasema hayo leo Novemba 24,2022 wakati wa hafla ya kugawa madume bora 50 ya ng’ombe aina ya boran kwa Vikundi vya wafugaji katika wilayan ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Waziri Ndaki amesema kuwa Dume moja ana uwezo wa kupanda majike 25 kwa mwaka, kwa vikundi vya wafugaji kwa lengo la kwenda kuboresha mifugo yao ambayo mingi ni ya asili.
“Mifugo mingi iliyopo hapa nchini ni ya asili na uzalishaji wake wa nyama na maziwa kwa mfugo ni ndogo, hivyo kwa kuanza kuboresha mifugo kwa kutumia madume haya pamoja na njia ya uhimilishaji kutasaidia wafugaji kuwa na mifugo michache ambayo itakuwa na uzalishaji mkubwa wa nyama na maziwa,” amesema
Aidha amesema kuwa Ng’ombe wa asili huzalisha nyama kilo 80 -120 kwa ng’ombe wakati baada ya kuboreshwa kwa kosaafu mfugaji anaweza kupata kilo 150 – 200 kwa ng’ombe.
Amesema kuwa pia kwenye upande wa maziwa ng’ombe hawa walioboreshwa kosaafu huwa na uwezo wa kutoa kati ya lita 5 – 10 za maziwa na hivyo kumfanya mfugaji apate tija zaidi tofauti na mfugaji wa ng’ombe wa asili. Waziri Ndaki amewataka Wafugaji kuyatunza madume hayo kwa kufuata taratibu zote wanazoelekezwa na wataalam wa mifugo.
''Navitaka vikundi ambavyo vimepatiwa madume hayo kuyatumia kwa kushirikiana na wafugaji wengine ili kuhakikisha tija inapatikana kwa wafugaji ndani ya Wilaya ya Chamwino.''amesisitiza
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Sekta ya Mifugo, Dkt. Asimwe Rwiguza amesema Wizara inaendelea kutekeleza mpango wa mabadiliko wa sekta hiyo ambapo licha ya kazi ya uboreshaji wa kosaafu inayoendelea, wafugaji wanaendelea kupatiwa elimu kuhusu malisho ya mifugo.
''Wizara inaendelea kuanzisha mashamba darasa ya malisho ya mifugo kwa lengo la kutoa elimu ya kilimo cha malisho na namna ya kuyatunza malisho hayo pamoja na nyanda za malisho ili malisho hayo yaweze kuwasaidia wakati wa kiangazi kikali.''amesema Dkt.Rwiguza
Naye Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mhe. Gift Msuya amesema kuwa wataenda kusimamia utekelezaji wa mpango wa mabadiliko wa sekta ya mifugo kwa kuhakikisha madume hayo yaliyogawiwa kwenye vikundi yanatunzwa na kutumika ili kuboresha kosaafu.
Awali Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko kutoka Sekta ya Mifugo, Bw. Stephen Michael amesema kuwa takribani asilimia 97 ya ng’ombe waliopo nchini ni wa asili hivyo katika kutekeleza mpango wa mabadiliko wa sekta, Wizara imepanga kununua mitamba 1,160,000 ambayo itapelekwa kwenye mashamba ya serikali.
Hata huvyo amesema kuwa kutokana na uzalishaji wake wafugaji wataweza kupata ng’ombe bora hapa nchini badala ya kutegemea kuagiza kutoka nje.
''Wizara inaendelea na zoezi la uhimilishaji mifugo ambapo tayari imeshapanga kuhimilisha takribani ng’ombe 373,000 katika mwaka wa fedha 2022/2023 kwenye maeneo ambayo hawatapata madume hayo.''amesema
Mwakilishi wa taasisi ya PASS Trust, Langelika Kalebi amesema kuwa taasisi hiyo ni mwezeshaji ikichochea maendeleo kwenye kilimo (mifugo, uvuvi, mazao, na mazao ya porini).
''Taasisi hiyo ipo nchi nzima ikichochea maendeleo kwenye upatikanaji wa mitaji na elimu, hivyo wanaongezea dhamana katika kurahisisha upatikanaji wa mitaji kwa mtu mmoja, vikundi, vyama vya ushirika.''amesema
Naye mwenyekiti wa wafugaji Wilaya ya Chamwino, Bw. John Kochocho ameishukuru serikali kupitia Sekta ya Mifugo kwa kuwapelekea wafugaji madume hayo ya ng’ombe yatakayokwenda kuboresha kosaafu na hivyo kuwafanya wazalishe kwa tija na kibiashara.
Serikali ya awamu ya sita ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefanikiwa kununua jumla ya madume bora ya ng’ombe wa nyama 366 aina ya Boran kama sehemu ya jitihada za kuendelea kuboresha tija ya ng’ombe tulionao nchini.
By Mpekuzi
Post a Comment