Brazil imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 Bora ya michuano ya kombe la Dunia baada ya kuifunga Switzerland ( Uswisi) 1-0 katika mechi ya kundi G.
Goli hilo pekee limefungwa na kiungo anayekipiga Manchester United Casemiro katika dakika ya 83 baada ya kupewa pasi na Vinicius.
Brazil imepata ushindi huo bila Neymar aliyeumia katika mechi ya kwanza dhidi ya Serbia ambayo Brazil ilishinda 2-0.
Brazil wanaongoza kundi hilo wakiwa na pointi sita, wakifuatiwa na Switzerland ( Uswisi) yenye pointi tatu.
Cameroon na Serbia wanafuata wakiwa na pointi moja kila moja baada ya kutoka sare 3-3 katika mechi yao ya leo.
Switzerland watahitaji kuwafunga Serbia ili wafuzu katika hatua hiyo.
Sare pia itatosha endapo Cameroon watashindwa kuwafunga Brazil.
MSIMAMO KUNDI G baada ya mechi mbili.
Brazil 6
Uswisi 3
Cameroon 1
Serbia 1
MECHI ZA MWISHO MAKUNDI
BRAZIL
vs
CAMEROON
USWISI
vs
SERBIA
KitengeSports
The post Brazil yafuzu 16 Bora appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment