Volcano kubwa kupata kutokea ndani ya kipindi cha miaka 40 imeripuka katika mji wa Hawaii.
Uji uji wa volcano hiyo umeanza kusambaa huku wakaazi wa eneo hilo wakipewa tahadhari juu ya kuenea kwa uji huo.
Mamlaka inayohusika na hali ya hewa nchini Marekani imesema kuwa huenda volcano hiyo , inayojulikana kama Mauna Loa ikasambaa zaidi.
Imepanda juu mita 4169 kutoka usawa wa bahari na kusambaa katika eneo lenye watani wa skweya mita 5,179.
Na hali imekuwa mbaya zaidi kufikia hatua ya kutolewa tahadhari.
Pia eneo hilo limepatwa na tetemeko la ardhi.
Hata hivyo, tahadhari ya wananchi wa eneo hiyo ya kuwataka kuhama bado haijatolewa.
Uji uji huo imeelezwa kwa unaweza kuleta athari ya kuharibu uoto wa asili, kuharibu mfumo wa usambazaji maji.
Kwa mujibu wa mamlaka za nchi hiyo, volcano hiyo imeripuka mara 33 katika mji huo toka mwaka 1984 .
Hata hivyo, licha ya hatari hiyo, idadi ya wakaazi wa eneo hilo imeongezeka mara mbili hadi kufikia watu 200,000.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa watu hao wapo katika hatari ya kuathiriwa na lava ya volcano hiyo.
The post Volcano kubwa yaikumba Hawaii appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment