ICAP YAPEWA SHAVU NA BUNGE UWEKEZAJI VIFAA TIBA NA AJIRA |Shamteeblog.

NA BALTAZAR MASHAKA,MWANZA 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi,Kifua Kikuu,Dawa za Kulevya na Magonjwayalisiyoambukiza,imesema Shirika la ICAP kwa kuwekeza kwenye vifaa na kutoa ajira kwa Watanzania linastahili kupongezwa.

Kauli hiyo imetolewa leo na  Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk.Alice Kaijage,kwa niaba ya wabunge wa kamati hiyo kutembelea miradi ya ICAP kujifunza inavyotekelezwa mkoani Mwanza.

Amesema ICAP kwa kuleta vifaa tiba Mwanza ikishirikiana na serikali lengo ni kuhakikisha afya za Watanzania zinaboreshwa pia imeajiri watu zaidi ya 400,ajira zinazowaingizia kipato kupitia miradi ya THIS 2022-23 na FIKIA+ kwa Ufadhili wa Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Rais wa Marekani wa Dharura wa Kupambana na Ukimwi (PERFAR).

“Kuwekeza kwenye utafiti,maabara,vifaa na fedha zaidi ya sh.bilioni  7 kwenye halmashauri mkoani Mwanza kusaidia shughuli za kuboresha afya,ICAP mmeisaidia serikali kufikia lengo la kuboresha afya za wananchi wake,”amesema Dk.Kaijage.

Ameshauri mradi wa FIKIA+ unaolenga kuimarisha huduma za kuzuia maambukizi mapya kwa kufanya tohara kinga kwa wanaume,huduma zinazo walenga mabinti wa rika balehe na wanawake vijana,uende mbali zaidi ili kuwaunganisha wasichana waunganishwe na SIDO wafanye ujasiriamali.

Wakiwa kwenye kituo cha MAT katika Hospitali ya Sekou Toure,Dk. Kaijage kwa niaba ya wabunge hao amesema serikali ina mpango wa kujenga makazi kwa Waraibu wanaotoka nje ya Mwanza na  nia njema ya kuwasaidia vijana wa makundi yote kupitia halmashauri ambapo imetenga ajira 200 na kushauri ajira hizo zitolewe kwa waraibu waliohitimu.

"Rais Samia na Serikali yake inatoa fedha kupitia vikundi,hivyo Waraibu watakaohitimu hapa waunde vikundi wakopeshwe mikopo ili wafanye shughuli za kiuchumi pia ujenzi wa MAT Kanda ya Ziwa wabunge washirikishwe,"amesema Makamu Mwenyekiti huyo.

Amesema Aidha Mratibu wa Ukimwi mkoani Mwanza,Dk.Pius Masele kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa,Dk.Thomas Rutachunzibwa,amesema ICAP kupitia Mradi wa FIKIA+ chini ya ufadhili wa PERFAR,inatumia sh.bilioni 3.5 kuwalipa mishahar na stahiki zingine watumishi 355 katika vituo vya kutolea huduma.

Pia halmashauri nane za mkoani Mwanza, hospitali za rufaa na binafsi zimetengewa zaidi ya sh. bilioni 2.3 kwa mwaka wa fedha 2022/23 kutekeleza afua mbalimbali za kudhibiti Ukimwi na tohara kinga.

Dk.Masele ameeleza mradi huo pia umetenga sh. bilioni 1.028 za kuendesha maabara ya vinasaba katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando huku halmashauri za Misungwi na Buchosa zikiwezeshwa magari mawili ya kufanya shughuli za afya.

Aidha kliniki ya Methadone (MAT) iliyoanzishwa Februari 2018 kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Serikali Marekani (PERFAR)kupitia CDC na ICAP inatoa huduma za uchunguzi wa magonjwa kwa Waraibu,ustawi wa jamii,kumwona daktari na tiba dawa ya Methadone kwa wajidunga.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sekou Toure ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza,Dk.Bahati Msaki amesema Waraibu 297 wanahudumiwa kituo cha MAT,wenye VVU ni 45 na wanaotumia ARV ni 21, homa ya ini B wapo 40 na homa ya ini C ni 38 ,waraibu 50 wamehitimu na 196 wamepata chanjo ya Uviko-19.

"Rais Samia Suluhu Hassan tunamshukuru kutuwezesha kupata kliniki hii na kuokoa maisha ya vijana wengi kwa kupata huduma ya tiba na kuna mwitiko mkubwa wa kuwapata vijana,rai yangu walioko mitaani waje kupata tiba waachane na matumizi ya dawa hizo,"ameshauri Dk.Bahati. SSSS






By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post