KWARESMA TUJIPATANISHA NA MUNGU |Shamteeblog.
Adeladius Makwega-Buigiri
Wakristo wametakiwa kubadilika na kujipatanisha na wenzetu na kufanya hivyo ni kujipatanisha na Mungu ambayo ndiye tunamkiri kama muumba wetu na mkombozi wetu ambaye hana hasira yoyote na mwanadamu, bali anahitaji kurudi kwake tunapomkosea, hayo yamesemwa na Padri Paul Mapalala, Paroko wa Kanisa la Bikira Maria Imakulata Parokia ya Chamwino Ikulu, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma katika misa ya Jumatano ya majivu ya Februari 22, 2023.
“Katika kipindi hiki cha Kwaresma kinachoanza kwa kupakwa mafuta kama Kanisa Katoliki linavyotangaza lazima tukiri wazi wazi kuwa mwanadamu ni kigeugeu anakubali hili leo na kesho anabadilika, badala ya kuwa waovu tuwe waponyaji, tujipatanishe na wenzetu na kujipatanisha na Mungu.”
Aliongeza kuwa siku arubaini za Kwaresma zitumike kwa kila Mkristo kujinoa zaidi katika neno la Mungu, kama haulewi uliza wanaolielewa neno hilo, wapo Mapadri, watawa wengine, makatekista na waaamini wengi tuwatumie wao kujifunza neno la Mungu.
Wengi wameziona Jumatano za Majivu nyingi, wengi wamepata mafundisho ya imani yetu, shida ni kutokumfuata Yesu Kristo. Mungu anatambua siri zetu, kubwa ni kila mmoja kutekeleza majukumu yake ya kiroho alisema,
“Tuiombee Parokia Yetu na bila kusahau kuliombea taifa letu hasa katika kipindi hiki cha Kwaresma siku zote arubaini.”
Mwandishi wa ripoti hii alishuhudia mara baada ya mahubiri hayo waamini hao walijongea mbele na altare na kupakwa majivu katika paji la uso ikichorwa ishara ya msalaba huku zikiimbwa nyimbo kadhaa zilionesha kuwa sasa Kipindi cha Kwaresma kimeanza.
Mpaka Misa hiyo Jumatano ya majivu iliyoanza saa 11.00 Jioni inamaliziku siku nzima ya Februari 22, 2023 ilikuwa ya jua kali mno katika eneo la Chamwino Ikulu sasa baadhi ya majani ya mahindi ukiyatazama yanaonesha rangi ya kaki huko ni kukauka wakati mengi hayajabebe chochote. Kutokana jua kali pia ardhi imekuwa kavu sana hata baadhi ya wakulima wameacha kupalilia mashamba yao wakingoja mvua kunyesha ili kupungua ukavu wa ardhi iwe laini ndiyo waendelee na palizi.
By Mpekuzi
Post a Comment