Ligi kuu ya soka ya NBC Tanzania bara inaendelea tena leo Februari 21, 2023 ambapo Simba watacheza na Azam FC katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa moja jioni.
Simba wanarejea katika ligi kuu wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza 3-0 dhidi ya Raja Casablanca katika mechi ya hatua ya makundi ya ligi ya Mabingwa barani Afrika.
Azam FC ndio timu pekee iliyochukua alama zote tatu mbele ya Mnyama kwenye Ligi msimu huu na leo watachuana katika mchezo wa raundi ya pili.
Smba ipo nafasi ya 2 ikiwa na pointi 53 baada ya michezo 22 huku Azam wakiwa nafasi ya 4 wakiwa na pointi 43 baada ya michezo 22.
Kuelekea mechi hiyo, beki wa Simba Shomari Kapombe amesema kubwa wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo.
” Tunahitaji pointi tatu muhimu ili kujiweka sawa katika mbio za ubingwa,” amesema Kapombe.
Baada ya mchezo huu Simba SC itakabiliana na miamba ya Uganda, Vipers SC kwenye mchezo wa raundi ya tatu wa hatua ya makundi mechi ambayo pia imebeba hatima ya Simba SC kuvuka hatua ya makundi.
The post Simba katika kibarua kigumu dhidi ya Azam appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment