Matajiri Qatar waitolea macho Man United |Shamteeblog.

Familia ya kifalme ya Qatar imeripotiwa kuwa na mpango wa kutaka kuinunua klabu ya Manchester United ya Uingereza wiki ijayo.

Tayari familia hiyo imewasilisha mpango wake huo katika benki ya Raine Group, ambayo ndio inasimamia mchakato wa uuzaji wa timu hiyo.

Benki hiyo pia imeitaka familia hiyo ya kitajiri kuwasilisha maombi yake mapema wiki ijayo, ingawa kuna habari zinazosema kuwa familia hiyo haipo tayari kutoa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kuinunua timu hiyo.

Familia ya Glazer ( pichani) ambayo ndio inamiliki timu hiyo kwa sasa inadaiwa kutaka kiasi cha paundi bilioni 6 wakati thamani ya klabu hiyo kwa sasa katika soko la hisa la Marekani ni paundi bilioni 3.2.

Qatar imeweka wazi jitihada zake za kutaka kuteka sekta ya michezo duniani, baada ya kufanikiwa kuandaa michuano ya kombe la Dunia kwa mafanikio.

The post Matajiri Qatar waitolea macho Man United appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post