Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kuwa Serikali isimamie msiba wa Watu 17 waliofariki kwa ajali Tanga hadi utakapomalizika.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amesema baada ya agizo hilo la Rais tayari hadi sasa Majeneza 16 yameshakamilika ambapo bado mawili mafundi wanaendelea nayo ikiwemo la Atanas Mrema ambaye alikuwa anasafirishwa kwenda kuzikwa Kilimanjaro na baada ya ajali jeneza alilobebewa likapasuka.
Aidha RC Mgumba amesema kuwa tayari wameshapata magari mawili kwa ajili ya kusafirisha miili hiyo ambapo kwa sasa wanasubiri maelekezo ya Familia.
"Tuliwapa pumziko kidogo Familia kwasababu wana mambo mawili kuna maiti zipo mochwari na kuna majeruhi wako Hospitali, kwahiyo tulitaka utulivu wao sasa hivi tunaenda kukaa nao ili tuone kwa pamoja kama wapo tayari kusafiri leo au wapo tayari kusafiri kesho"
from Author
Post a Comment