Staa wa Zamani wa Newcastle Anatafutwa Kwenye Kifusi Uturuki |Shamteeblog.



Staa wa zamani wa vilabu ya Chelsea na Newcastle vya England Christian Atsu (31) Raia wa Ghana ambaye kwa sasa anacheza Hatayspor ya Uturuki amekwama kwenye kifusi cha jengo lililoanguka baada ya tetemeko la ardhi.


Harakati za kumuokoa Atsu zinaendelea lakini kwenye tetemeko hilo lililotokea leo nchini Uturuki mitandao mbalimbali imeripoti kuwa watu zaidi ya 1400 wamefariki Dunia.


Atsu ambaye alijiunga na Chelsea 2013 na kuishia kutolewa kwa mkopo Newcastle na Everton, alikuwa sehemu ya mchezo wa Ligi Kuu Uturuki jana kati ya timu yake ya Hatayspor dhidi ya Kasimpasa ambapo aliisaidia kupata ushindi wa 1-0 akifunga goli dakika ya 90+7.



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post