TFF yaufungia ‘Shamba la Bibi’ |Shamteeblog.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungia uwanja wa Uhuru, maarufu ‘Shamba la Bibi’ uliopo jijini Dar es Salaam kwa kukosa vigezo vya kuchezewa mechi za ligi.

Hii ni baada ya miundombinu yake kutokidhi matakwa ya kanuni.

Kufuatia uamuzi huo, timu zote zinazotumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani zimetakiwa kutumia uwanja mwingine mpaka uwanja huo utakapofunguliwa, baada ya kufanyiwa marekebisho na kukaguliwa na TFF.

The post TFF yaufungia ‘Shamba la Bibi’ appeared first on Kitenge Blog.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post