Uchambuzi Mechi ya Yanga na Tabora United, Matumizi Makubwa ya Nguvu Yalitawala |Shamteeblog.




Mchezo ulikuwa na matumizi makubwa ya nguvu . Takwimu zinadhibitisha hilo , kulikuwa na FAUL nyingi sana : Tabora walikuwa vizuri sana kwenye kiungo walicheza kwa utulivu mkubwa then walizuia kwa ufanisi mzuri .

Miguel Gamondi na mabadiliko ya kikosi kutoka mchezo uliopita dhidi ya Medeama na huu : 2-1-5-2 wakianza mpira nyuma (Sure mbele ya Job na Bacca huku Kibwana na Kibabage wanasoge juu ….. dhumuni lilikuwa ni nini ?

Kibabage na Kibwana wakisogea juu maana yake Yanga wanakuwa na namba 10 wawili ndani Maxi na Aziz then Moloko anakuwa pembeni zaidi , Yanga waliweza kuifungua Tabora vizuri sana kupitia pembeni ya uwanja “Flanks” : Nafikiri Yanga walikosa pasi za kuifungua Tabora “Penetration Pass” mda mwingi walitumia mipira ilikufa na Cross .

Tabora walicheza vizuri sana , pasia mpira kwa usahihi , utulivu kwenye mpira then walikuwa tayari kwenye mapambano ya 50/50 : Nafikiri Tabora walikosa ufundi wa kuifungua defense ya Yanga , hawakuwa na utulivu na maamuzi kwenye nusu ya mpinzani .

NOTE:

Aziz Ki magoli 10 mpaka sasa kwenye NBCPL : Msimu bora 🔥

Kibabage ameboresha sana uchezaji wake 👏 Kasi , Utulivu na maamuzi .

Yule namba 8 wa Tabora 🔥 Najim ✅

FT: Tabora United 0-1 Yanga .

By Kelvinrabson_



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post