Imebainika wanawake asilimia 2.1 pekee ndio walijitokeza Katika kuwania nafasi za uongozi wa vijiji jambo ambalo limewaamsha wanaharakati kuona umuhimu wa kuwekeza juhudi za ziada ili kuondokana na hali hiyo kwa lengo la kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa kijinsia.
Hayo yamebainishwa leo Oktoba 23,2024 na Afisa Idara ya Mafunzo TGNP Anna Sangai kwenye semina za jinsia zinazofanyika kila Jumatano TGNP-MTANDAO Mabibo Jijini Dar es Salaam.
Amesema licha ya kutimia miaka 29 tangu mkutano wa Beijing ulipofanyika takwimu bado zinaonesha hali sio nzuri hata katika nafasi za uongozi wa vijiji kwani wanawake ni Asilimia 2.1 pekee.
Aidha Sangai ametoa Rai kwa wanawake waliowania nafasi za uongozi ambao kwa bahati mbaya hawatapita, wanatakiwa kutoa changamoto na vikwazo walivyopitia wakiwa wanagombea nafasi hizo.
Kwa upande wake, Mwanaharakati wa Jinsia Nelson Munisi ameshauri kuwa mwanamke anapaswa kutazamwa kwa jicho la kipekee Kama ilivyo katika nafasi za ubunge wa viti maalumu kwa lengo la kuleta usawa wa kijinsia Katika uongozi.
By Mpekuzi
Post a Comment