MGOGORO WA UONGOZI NDANI YA CHADEMA KANDA YA KASKAZINI? |Shamteeblog.

Taarifa za hivi karibuni kutoka Chadema zinaonyesha kuwepo kwa mvutano wa madaraka kati ya Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, na Katibu wake, Amani Golugwa. Mgogoro huu umeonekana wazi wakati Mwenyekiti wa kanda alipoitisha mkutano na waandishi wa habari, huku Katibu akitoa taarifa kuhusu kuanza kwa uchaguzi wa ndani wa chama Kanda ya Kaskazini. 

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Oktoba 23, 2024, uongozi wote wa wilaya ya Longido na mkoa wa Arusha umepigwa chini kwa madai ya utovu wa nidhamu na kukiuka maadili ya chama. 

Uamuzi huu ulifanywa baada ya tukio la Oktoba 22, 2024, ambapo viongozi waliodaiwa kushindwa kusimamia uchaguzi wa ndani kwa haki walihusishwa na vitendo vya kihuni.

Kuvunjwa kwa uongozi huu kunadhihirisha mgongano wa kimkakati kati ya uongozi wa kanda chini ya Godbless Lema na maamuzi kutoka ofisi ya Katibu Amani Golugwa. Hali hii inakuja wakati ambapo mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji, na vijiji ukiendelea, na vyama vingine vikiwa katika maandalizi thabiti.




 



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post