
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Kagera Mhe Nazir Karamagi akizungumza katika hicho
Na Lydia Lugakila - Bukoba
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa Kagera Nazir Karamagi amewaomba Wanakagera kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumpa kura za Kishindo kama shukrani ya Mkoa huo kwa jinsi alivyouzawadia miradi mingi ya Maendeleo.
Mhe, Karamagi ametoa kauli hiyo katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika Februari 19,2025 katika Ofisi za Mkoa huo.
Amesema kuwa wanakagera wanatambua kazi kubwa aliyoifanya Rais Samia ikiwemo kuuinua Mkoa huo kiuchumi hivyo wampe kura nyingi kama zawadi.
Mwenyekiti huyo amesema Rais Samia amefanya mambo mengi na makubwa hasa katika miradi mbali ikiwemo sekta ya maji, Barabara, umeme na mingine mingi.
Aidha amewashukuru wadau mbali mbali pamoja na viongozi jinsi walivyo wezesha chama hicho ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Serikali za mitaa huku akiwaomba kumpigia kura za kutosha Rais Samia katika uchaguzi mkuu ujao 2025 pia Wadiwani na Wabunge.
Amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe Hajat Fatma Mwassa kwa namna alivyobadili taswira ya Mkoa huo hasa katika ubunifu ulioufanya Mkoa huo kubadilika.
By Mpekuzi
Post a Comment