Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ametangaza kuanza kwa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA na Miaka 50 ya Utoaji Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
Akizungumza Machi 05, 2025 Jijini Dar es Salaam na Waandishi wa Habari Prof. Mkenda amesema kuwa Maadhimisho hayo yanafanyika wakati Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo ya kuhakikisha Vyuo vya VETA venye hadhi ya Mikoa vinajengwa katika Mikoa yote na vya hadhi ya Wilaya vinajengwa katika Wilaya zote nchini.
Prof. Mkenda amesema katika kutekeleza agizo hilo Serikali inakamilisha Chuo cha VETA katika Mkoa wa Songwe ambao haukuwa na chuo hicho na pia kuendelea na ujenzi wa Vyuo vya wilaya 64 katika wilaya ambazo hazikua na vyuo vya VETA.
By Mpekuzi
Post a Comment