Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT-Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman akihutubia wananchi mkoani Shinyanga.
Na Mwandishi Wetu, Malunde 1 Blog Shinyanga
Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Taifa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema kuwa chama chake kiko tayari kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kwa dhamira thabiti ya kuendeleza harakati za mabadiliko ya kweli, haki kwa wananchi, na ukombozi wa Taifa.
Akihutubia wananchi katika viwanja vya shule ya Msingi Town iliyopo Manispaa ya Shinyanga Mei 24, 2025, Mheshimiwa Othman ameweka wazi kuwa dhamira ya kuasisi Taifa hili ilikuwa ni kuwapatia wananchi uhuru, sauti, na heshima katika kufanya maamuzi ya taifa lao – dhamira ambayo inazidi kudhoofishwa na mfumo wa sasa wa uongozi.
"Ndugu wananchi, lile ambalo tulilipambania sasa halipo tena, na wenzetu ndio ambao wamelipoteza," amesema kwa msisitizo, akirejea misingi ya uhuru na usawa wa wananchi.
Mheshimiwa Othman ameongeza kuwa kunyima wananchi haki ya kupaza sauti na kuchagua viongozi wanaowataka ni sawa na kuwafanya kuwa watumwa katika nchi yao wenyewe.
"Pale ambapo wananchi hawana sauti wala haki ya kuchagua wanaowaamini, Taifa hubaki dhaifu na tegemezi – hali ambayo siyo stahiki ya Watanzania," amesema Mheshimiwa Othman.
Mheshimiwa Othman pia ameeleza kuwa licha ya Mkoa wa Shinyanga, na maeneo ya jirani, kubarikiwa na rasilimali nyingi kama dhahabu na almasi bado, rasilimali hizo zimekuwa zikitumiwa vibaya, huku wananchi wa maeneo hayo wakibaki maskini.
"Shinyanga kama ingekuwa nchi inayojitegemea, ingeweza hata kuikopesha Tanzania nzima," aamesema Othuman.
Ameongeza kuwa wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakihadaiwa na kushawishiwa kila msimu wa uchaguzi, lakini hali halisi haibadiliki kwao.
Ziara ya Mheshimiwa Othman ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ya ACT-Wazalendo inayoitwa Operesheni Linda Demokrasia, inayolenga kufufua matumaini ya wananchi na kuhakikisha kuwa sauti zao zinasikika kupitia sanduku la kura.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ndugu Ado Shaibu, amempongeza Mhe.Othman kwa kuwa kiongozi asiye na chembe ya kuyumba katika misingi ya haki huku akiwapokea wanachama 26 walio jiunga na chama hicho kutoka katika vyama vingine vya upinzani .
Mkutano huo wa kisiasa umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kanda ya ziwa, akiwemo Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mkoa wa Shinyanga, Ndugu Hassan Ibrahim, pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT-Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman akihutubia wananchi wa mkoa wa Shinyanga.
Wananchi wa mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT-Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman wakati wa mkutano.

Katibu mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Taifa , Ndugu Ado Shaibu, aa cha ACT-Wazalendo Taifa Shangwe Ayo akizungumza na wananchi wa mkoa wa Shinyanga wakati wa mkutano nakupokea wanachama wapya 26 waliohama vyama vyao na kujiunga na ACT Wazalendo.
Wananchi wa mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT-Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman wakati wa mkutano.
Katibu Mwenezi wa Chama cha ACT-Wazalendo Taifa Shangwe Ayo akizungumza na wananchi wa mkoa wa Shinyanga wakati wa mkutano.
Wananchi wa mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT-Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman wakati wa mkutano.
Wananchi wa mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT-Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman wakati wa mkutano.
Wananchi wa mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT-Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman wakati wa mkutano.

Wananchi wa mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT-Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman wakati wa mkutano.
Wananchi wa mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT-Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman wakati wa mkutano.
By Mpekuzi
Post a Comment