CHAMA CHA WALIMU TANZANIA CHAPATA VIONGOZI WAKE |Shamteeblog.

Bi. Sharifa Mngwali(Mwakilishi  wa wenyeviti wa kitengo cha walimu wanawake)

Sharifa Hatibu Mngwali

NA. ELISANTE KINDULU, DODOMA.

CHAMA cha walimu Tanzania (CWT) kimehitimisha uchaguzi wake leo alfajiri mjini Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre kwa kupata viongozi wa kitaifa watakaohudumu kwa kipindi cha mwaka 2025-2030.

Wajumbe 913 wa mkutano mkuu walioketi jana waliwachagua viongozi mbalimbali na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:

Seleman Ikomba (Rais wa chama) kura 608, Shaban Ambindwile(Makamu wa Rais) kura 236, Joseph Misalaba(Katibu Mkuu) kura 742, Protas Magesa(Naibu Katibu Mkuu) kura 391 na Nashon Kidudu (Mweka Hazina) kura 913.

Wengine ni Pili Omari (Mwakilishi wa walimu vijana), Shani Ulumbi (Mwakilishi wa walimu wenye ulemavu) na Elizabeth Werema (Mwakilishi  wa walimu wanawake).

Nafasi ya wadhamini wa Chama imechukuliwa na Ally Mketo, Evod Enerico na Mwamaja wakati Proper Mutungi ameshinda nafasi ya mwakilishi wa TUCTA Taifa.

Uchaguzi huo ulitanguliwa na ule wa walimu wa kitengo cha walimu wanawake ambapo Bi. Sharifa Hatibu Mngwali alichaguliwa kuwa Mwakilishi wa wenyeviti wa kitengo cha walimu wanawake kwa kupata kura 240 dhidi ya Agness Nyamsusa (79) na Oliva Mangu (16).

Wajumbe wa kamati ya walimu wanawake ilichukuliwa na  Mwl. Tenisia Katukuru, Mwl. Lulu Njau, Mwl. Fortunata Muyanga, Mwl. Mgode, Mwl. Matambo na Mwl. Edina.

Mkutano Mkuu wa Chama hicho ulifunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh. Doto Mashaka Biteko kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mh. Samia Suluhu Hassan.

Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu, kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu, Mh. Ridhiwani Jakaya Kikwete na viongozi wengine wa Serikali.




By Mpekuzi

Post a Comment

Previous Post Next Post