UWANJA WA NDEGE KIA KUWA LANGO LA WATALII. |Shamteeblog.

NA FARIDA SAID MOROGORO

Wizara ya maliasili na utalii imesema inampango wa kuufanya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA kuwa lango la kuingilia watalii kutoka nchini mbalimbali wanakuja kujionea vivutio na upekee wa Tanzania. 

Wizara imeweka mikakati wa kuongeza watalii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wa sekta ya usafirishaji ili kufia adhima ya serikali ya awamu ya tano ya kufikisha watalii milioni tano kwa mwaka ifikapo 2025.

Hayo yamesemwa na waziri wa maliasili na utalii Dkt. Damas Ndumbaro katika mkutano na wadau wa utalii katika sekta ya usafirishaji ambapo ameitaja sekta usafirishaji kuwa mhimili mkubwa wa kuongeza idadi ya watalii nchini. 

Waziri ndumbaro amesema ili watalii kutoka nchi mbalimbali waweze kufika katika hifadhi zetu ni lazima watumie usafiri wa ndege ama meli,hivyo watawasiliana na wizara ya uchukuzi ili kuona namna ya kuweza kupunguza kodi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA.

Kwa upande wake kaimu Kamishna wa uhifadhi wa mamlaka ya usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) Mabula Misungwi, amesema wao kama TAWA wamepokea ushauri wa wadau wa utalii na kuahidi kuyafanyia kazi mapendekezo ya wadau ili kukuza sekta ya utalii wa uwindaji.

Amesema Tanzania inaongoza kwa rasilimali na vivutio vingi ambavyo vingine havipatikani katika maeneo mengine yeyoyote duniani huku akiwataka watalii kutembelea hifadhi za taifa.





By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post