BADRU: HESLB ITAENDELEA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI |Shamteeblog.

 

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Abdul-Razaq Badru akizungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku ya huduma kwa wateja yaliyoanza tarehe 12-16 April mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka  Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Albert Rukeisa akitoa mada wakati wa mafunzo  ya siku tano ya huduma kwa wateja yaliyoanza tarehe 12- 16 April mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

(NA MPIGAPICHA WETU)

 ………………………………………………………………………………………….

Na Mwandishi Wetu,HESLB

DAR ES SALAAM

13 April, 2021

 

MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru amesema HESLB imejipanga kutekeleza malengo iliyojiwekea katika Mpango Mkakati wa Taasisi hiyo ili kuendelea kutoa  huduma bora kwa wananchi

Akizungumza leo (Jumanne April 13, 2021) Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya huduma kwa wateja yaliyoandaliwa kwa watumishi wa Ofisi hiyo, Badru alisema kwa kuzingatia umuhimu huo HESLB itaendelea kuwajengea uwezo watumishi wote ili kuwaongezea ujuzi, maarifa na ubunifu.

“Kama mnavyokumbuka tunatelekeleza Mpango Mkakati wa Miaka mitano wa Taasisi uliojikita katika kuimarisha huduma na mifumo yetu ya kiutendaji ndani ya taasisi, hivyo suala la mafunzo kwa watumishi litaendelea kupewa kipaumbele na HESLB kadri inavyowekezana” alisema Badru.

Aidha Badru alisema mafunzo hayo ni moja ya juhudi za HESLB za kuimarisha mahusiano ya wadau na wateja wa taasisi hiyo na hivyo kuwataka watumishi hao kutumia fursa hiyo kujiongezea ujuzi,maarifana ubunifu ili kujenga taswira chanya taasisi hiyo.

Akifafanua zaidi Badru alisema HESLB imezidi kujiimarisha kiutendaji, ambapo imeendelea kupokea watumishi wa kada mbalimbali kutoka katika taasisi na idara mbalimbali za Serikali hatua iliyoiwezesha taasisi kuendelea kutimiza malengo iliyojiwekea katika kutoa hudumakwawateja

“HESLB imebeba maslahi mapana zaidi kwa makundi mbalimbali ya kijamii,tunapaswa kutambua wajibu tulionao katika kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji lakini pia kuongeza kasi ya ukusanyaji wa madeni, tunapaswa kufikia malengo haya”  alisema Badru

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha na Utawala HESLB, Neema Kuwite alisema mafunzo hayo ya siku tano yanashirikisha jumla ya watumishi 25 kutoka Ofisi ya HESLB Dar Salaam, Dodoma, Arusha, Mtwara, Mwanza, Zanzibar na Mbeya.

“Mafunzi haya ni ya awamu ya pili, awamu ya kwanza ilifanyika mwezi machi ikihusisha jumla ya watumishi 25, mafunzo haya ni endelevu na kila mtumishi wa HESLB atapatiwa mafunzo haya’ amesema Kuwite.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post