Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mary Maganga akifungua Kikao cha Wadau wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji wa bidhaa zinazofungashwa kwa chupa za plastiki za rangi kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mtumba jijini Dodoma leo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mohammed Abdallah Khamis (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Dkt. Andrew Komba wakiwa katika kikao cha Wadau wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji wa bidhaa zinazofungashwa kwa chupa za plastiki za rangi kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mtumba jijini Dodoma leo.
Wadau wakiwa katika kikao cha Wadau wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji wa bidhaa zinazofungashwa kwa chupa za plastiki za rangi wakiwa katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mtumba jijini Dodoma leo.
Afisa Mipango Miji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Hussein Omar (nyuma), Afisa Sera kutoka Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI) Anna Kimario na Afisa Mazingira Joseph Kiwango wakiwa katika kikao cha Wadau wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji wa bidhaa zinazofungashwa kwa chupa za plastiki za rangi kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mtumba jijini Dodoma leo.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
………………………………………………………………………………
Makampuni yanayozalisha bidhaa zinazofungasha chupa za plastiki zimepewa wiki moja kuandaa mikakati inayotekelezeka ya muda mfupi na mrefu itakayoonesha udhibiti wa chupa za plastiki wanazozizalisha na kuiwasilisha katika Ofisi ya Makamu wa Rais Aprili 20, 2021.
Agizo hilo limetolewa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga wakati akifungua Kikao cha Wadau wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji wa bidhaa zinazofungashwa kwa chupa za plastiki za rangi kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mtumba jijini Dodoma leo.
Maganga alibainisha kuwa uchafuzi wa mazingira utakanao na chupa za plastiki zenye rangi umekuwa changamoto nchini. Aidha, katika kukabiliana na changamoto hizo kuna haja ya wazalishaji kutimiza wajibu wao wa kuziondosha katika mazingira ikiwemo kuzirejeleza kama Sheria ya Mazingira inavyoelekeza.
“Kutokana na umuhimu wa udhibiti wa taka za plastiki tunao wajibu wa kuungana pamoja ili kuwa na juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto za udhibiti wa taka zitokanazo na plastiki kama Kanuni ya 4 ya Kanuni za Usimamizi wa taka ngumu za mwaka 2009 chini ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 zinavyoelekeza,” alisema.
Hivyo kwa mujibu wa kanuni hizo ni kuwa mzalishaji anao wajibu wa kuondosha kwenye mazingira taka zitokanazo na bidhaa anazozalisha (Extended Producer Responsibility).
Katibu Mkuu Maganga alifafanua kuwa pamoja na jitihada za kuziondosha chupa hizo katika mazingira bado kumekuwa na changamoto ya kukosekana kwa makampuni ya kutosha yanayojishughulisha na urejelezaji wa chupa hizo.
Kutokana na changamoto hiyo alisema chupa hizo zimeendelea kuzagaa katika mazingira yetu na hivyo kuchangia uchafuzi wa mazingira ikilinganishwa na chupa zisizo na rangi.
“Natoa wito kwa jamii kukabiliana na changamoto za udhibiti wa taka zitokanazo na plastiki ambapo mzalishaji ana wajibu wa kuondosha kwenye mazingira taka zitokanazo na bidhaa anazozalisha,” alisisitiza Maganga.
Kikao hicho kimeshirikisha wawakilishi kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), mwakilishi kutoka Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI) na wawaskilishi wa wamiliki wa viwanda.
By Mpekuzi
Post a Comment