Mkuu wa wilaya ya Kigoma Rashid Chuachua akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wafanyabiashara wa mkoa Kigoma iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Naibu Kamishna wa forodha na ushuru wa bidhaa TRA Makao Makuu, Julieth Nyomolelo
Naibu Kamishna wa forodha na ushuru wa bidhaa TRA Makao makuu Julieth Nyomolelo (kulia) akikabidhi tuzo kwa mfanyabiashara wa mkoa Kigoma Kilahumba Kivumo (kushoto) ambaye amekuwa mmoja wa wafanyabiashara waliofanya vizuri mkoani Kigoma
Sehemu ya wafanyabiashara na wageni waliohudhuria utoaji tuzo kwa wafanyabiashara wa mkoa Kigoma waliofanya vizuri katika ulipaji kodi
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MKUU wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amekemea wafanyabiashara wa mkoa huo wanaoingiza bidhaa nchini kupitia ziwa Tanganyika bila kufuata taratibu wa kulipa ushuru (Magendo) wamekuwa wakiikosesha serikali mapato na hivyo kutoa onyo kwamba adhabu kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Andengenye alisema hayo katika hafla ya utoaji tuzo kwa wafanyabiashara wa mkoa Kigoma iliyoandaliwa na Mamlaka ya mapato kutambua mchango mkubwa wa wafanyabiashara hao katika kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati hivyo kuifanya mamlaka hiyo kufikia lengo la ukusanyai.
Pamoja na kutoa onyo hilo Mkuu wa wilaya Kigoma, Dk.Rashid Chuachua ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma alisema kuwa anaipongeza TRA kwa kazi kubwa ya kukusanya kodi na kufikia malengo ya ukusanyaji yaliyowekwa jambo ambalo linaifanya serikali kuweka mazingira wezeshi ya kuifanya mamlaka hiyo kutimiza malengo yake kwa ufanisi.
Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya Kigoma Rashid Chuachua alisema kuwa ukwepaji kodi sambamba na wafanyabiashara wasiotumia mashine za kielektroniki kumesababisha serikali kupoteza mapato hivyo amepota onyo kwa wafanyabiashara wanaofanya hivyo kuacha mara moja huku akiipongeza TRA kuongeza ukusanyaji mapato ambako kumeifanya serikali kutekeleza miradi mikubwa Kwenda kwa wananchi.
Akizungumza katika hafla hiyo Naibu Kamishna wa forodha na ushuru wa bidhaa TRA Makao Makuu, Julieth Nyomolelo amesema kuwa uingizaji wa bidhaa nchini bila kulipiwa kodi kwa njia ya magendo imekuwa changamoto kubwa ambayo inavuruga malengo ya mamlaka hiyo katika kufikia lengo la ukusanyaji mapato nchini.
Naibu Kamishna wa forodha na ushuru wa bidhaa alisema kuwa ulipaji kodi kwa hiari kwa kufuata taratibu za kisheria kulingana na biashara iliyofanyika inatija kubwa katika kuongeza makusanyo ya mamlaka hiyo sambamba na kufikia au kuvuka lengo lililoweka hivyo ametoa wito kwa watu wote kufuata taratibu na kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati.
Mmoja wa wafanyabiashara waliopewa tuzo kwenye hafla hiyo, Kilahumba Kivumo alisema kuwa mabadiliko ya utendaji ya maafisa wa TRA ambayo yametokana na vikao vya mara kwa mara wanavyofanya imekuwa chachu kwa wafanyabishara kulipa kodi kwa hiari na kuwaita maafisa hao kuwapa ushauri badala ya kuwakimbia.
By Mpekuzi
Post a Comment