MSIGOMBANISHE WANANCHI NA SERIKALI YA CCM – ODDO MWISHO |Shamteeblog.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Kilian Mwisho akizungumza na Wananchi na Wanachama wa kata ya Mlingoti Wilayani Tunduru wakati wa kuhitimisha ziara yake Tunduru Kusini na Kaskazini
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Kilian Mwisho akizungumza na Wananchi na Wanachama wa kata ya Mlingoti Wilayani Tunduru wakati wa kuhitimisha ziara yake Tunduru Kusini na Kaskazini
Wananchi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Ruvuma Wilayani Tunduru waliojitokeza kumsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Kilian Mwisho
Wananchi wa Kata ya Lukumbule Wilayani Tunduru waliojitokeza kumsikiliza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Kilian Mwisho
Wananchi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Mtina Wilayani Tunduru waliojitokeza kumsikiliza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho

Na Regina Ndumbaro Tunduru

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Oddo Kilian Mwisho, amekamilisha ziara yake ya kata kwa kata wilayani Tunduru, ambapo amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wakulima na wananchi kuhusu changamoto zinazowakabili.

Moja ya changamoto kubwa iliyobainishwa ni ucheleweshaji wa pembejeo za ruzuku, hususan salfa, na ukosefu wa elimu sahihi kuhusu matumizi ya dawa za kupulizia korosho.

Oddo ameitaka Bodi ya Korosho wilayani humo kuhakikisha pembejeo zinawafikia wakulima kwa wakati ili kuongeza tija katika kilimo cha zao hilo muhimu kwa uchumi wa wakulima wa maeneo hayo.

Aidha, Oddo amesisitiza kuwa serikali inafanya juhudi kubwa kuhakikisha uhakiki wa wakulima wote wa korosho unafanyika ipasavyo ili kupata takwimu sahihi za uzalishaji.

Amebainisha kuwa baadhi ya changamoto zinazokwamisha maendeleo ya kilimo ni wataalamu wa sekta ya kilimo kushindwa kufika maeneo husika ya wakulima na ucheleweshaji wapembejeo hizo za salfa.

Katika juhudi za kuboresha sekta hiyo, amewataka wakulima kutoa taarifa sahihi kuhusu hali ya mashamba yao ili kuwezesha serikali kuchukua hatua stahiki kwa maendeleo yao.

Katika hotuba yake, Oddo amekemea vikali vitendo vya baadhi ya viongozi wa chama kutoweka vikao na wananchi kujadili changamoto zinazowakabili.


Ameeleza kuwa CCM ni chama madhubuti tangu mwaka 1977, lakini baadhi ya viongozi wa ngazi za chini wamekuwa wakishindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo, jambo ambalo linakwamisha maendeleo ya wananchi na wanachama.

Amehimiza viongozi hao kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kuwahudumia wananchi kwa uadilifu na uwajibikaji wa hali ya juu.

Pamoja na hayo, Oddo ameonya dhidi ya uchochezi unaofanywa na baadhi ya vyama vya upinzani na wanachama wenyewe kwa lengo la kukichafua CCM na serikali yake.

Ameitaka jamii kupuuza maneno ya uchochezi na badala yake kuendelea kuiunga mkono serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambayo imefanikiwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa wananchi.


Ametaja mafanikio makubwa katika sekta za miundombinu, ya umeme,elimu,barabara na maji, akibainisha kuwa serikali ina mpango wa kuhakikisha kila kitongoji nchini kinapata umeme wa uhakika.

Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Ruvuma amesisitiza umuhimu wa kudumisha amani na mshikamano nchini, akiwataka wananchi kuepuka kurubuniwa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi.

Ameeleza kuwa chama na Serikali zina utaratibu wake wa kushughulikia changamoto za wananchi, hivyo ni muhimu kwa wananchi na viongozi kushirikiana kwa pamoja ili kuleta maendeleo endelevu.


By Mpekuzi

Post a Comment

Previous Post Next Post