WASIRA AFUNGUA OFISI MPYA YA CCM ILIYOJENGWA NA KATAMBI! APONGEZWA KUHESHIMU NA KUIMARISHA CHAMA! |Shamteeblog.

Na mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ameonesha uongozi bora na kujitolea kwa kujenga ofisi za CCM katika Kata ya Chibe, hatua inayothibitisha dhamira yake ya kuimarisha chama na kusaidia jamii. 

Leo, Machi 26, 2025, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amefungua rasmi ofisi mpya ya CCM katika kata hiyo, akimpongeza Mbunge Katambi kwa juhudi za kipekee katika kuendeleza chama na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Ofisi hii ni miongoni mwa ofisi mbili zinazojengwa na Mbunge Katambi, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake za kuboresha miundombinu ya chama. Ofisi nyingine imejengwa katika Kata ya Ibadakuli.

 Wasira amesema kuwa ofisi hizi zitakuwa ni sehemu muhimu ya kuunganisha wananchi na serikali, kwa kutoa fursa ya kusikiliza maoni na kero za wananchi.

 Amesisitiza kuwa, CCM ni daraja linalounganisha serikali na wananchi, na ofisi hizi zitasaidia katika kufanikisha malengo ya chama na kuendeleza maendeleo.

Mjumbe wa NEC, Richard Kasesela, pia amepongeza uongozi wa Mbunge Katambi kwa kujitolea na kazi nzuri ya kuimarisha chama.

 Amesema ujenzi wa ofisi hizo ni ishara ya kuheshimu na kuimarisha CCM katika maeneo ya vijijini.

Katibu wa CCM Kata ya Chibe, Kasokila Kameja, amefafanua kuwa ujenzi wa ofisi hiyo ulianza Mei mwaka 2024 na kukamilika Novemba mwaka huo, kwa gharama ya shilingi milioni 51.7. 

Ameongeza kuwa ofisi hiyo imekuwa ni mkombozi mkubwa kwa shughuli za chama katika kata hiyo.





By Mpekuzi

Post a Comment

Previous Post Next Post