Na Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amejumuika na Wanashinyanga wakiongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Sheikh Ismail Habib Makusanya kumuombea Dua Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo pamoja dua maalum pia wamemuombea kheri, afya njema maisha marefu na yenye baraka zaidi ili aendelee kuwatumikia Watanzania wote wakiwemo Wanashinyanga.
Dua hii Maalum imefanyika nyumbani kwake RC Macha mara baada ya Iftar ambayo ilijumuisha viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita , Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Peter Masindi, viongozi wa dini, vyama vya siasa, Serikali na watoto wenye mahitaji maalum ambapo kwa upande wake alitumia nafasi hiyo kuwashukuru viongozi wote kwa dua hiyo njema kwa Mhe. Rais naye akamtakia heri na baraka zaidi ili aendelee kuwatumikia Wanashinyanga na Watanzania kwa ujumla.
RC Macha pia ametumia nafasi hiyo kuwashukuru pia Wafanyabiasha ambao awali katika kuelekea kuanza kwa mfungo mtukufu wa Ramadhan na Kwaresma aliwaomba kutopandisha bei ya bidhaa hasa vyakula vya nafaka kwa lengo la kujipatia faida zaidi jambo ambalo amesema walizingatia na hivyo hapakuwa na upandishaji wa bei kwa kipindi hiki chote.
"Ninawashukuru sana viongozi wote wa dini vyama vya siasa na watoto wetu wenye mahitaji maalum kwa kufanya dua hii maalum ya kumuombea Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan afya njema, kheri, baraka, maisha marefu na nguvu zaidi ili aweze kuendelea kuwahudumia Wanashinyanga na Watanzania wote kwa ujumla," amesema RC Macha.
Dua hii Maalum ya kumuombea Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekwenda sanjari na Iftar Maalum iliyowajumuisha Watoto wenye Mahitaji Maalum kutoka maeneo mbalimbali ya hapa Manispaa ya Shinyanga kwa niaba ya wote mkoani Shinyanga.
By Mpekuzi
Post a Comment