JESHI LA POLISI DODOMA KUMUENZI SHUJAA WA USALAMA BARABARANI IHUMWA |Shamteeblog.



Na Barnabas Kisengi, Dodoma

Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma limempatia vitendea kazi na elimu Elias Makasi ambaye kwa mwaka wa 18 sasa amekuwa akijitolea kuwavusha barabara wanafunzi wa shule ya msingi ya Jenerali Musuguri iliyopo Kata ya Ihumwa jijini Dodoma. 

Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo vyenye michoro ya alama za usalama barabarani pamoja na viakisi mwanga Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma (SACP) George katabazi amepongeza uongozi wa Shule hiyo kwa kumuamini mzee huyo na kuwasaidia kuwavusha wanafunzi pindi wanapoenda shuleni na kutoka na kuepuka ajali.

"Mzee Eliasi amekuwa mzalendo wa kweli kwa kuwasaidia wanafunzi hawa kuepukana na ajali zisizo za lazima sisi Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma tunamuunga mkono na tutampatia pia elimu ya usalama barabarani ili aendelee kuwanusuru watoto hawa na ajali za barabarani kutokana eneo hili kuzungukwa na makazi ya watu na vyombo usafiri kupita Karibu na shule,"amesema Rpc Katabazi.

Aidha katabazi amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kupitia kitengo cha usalama barabarani limeweka mikakati ya kuzifikia shule zote za mijini na vijijini hususani shule za msingi zilizopo kwenye makazi watu na kuziwazesha vifaa vya vyenye michoro ya usalama barabarani pamoja na elimu itakayo saidia kulinda kizazi hicho cha wanafunzi na ajali za barabarani.

Vilevile Katabazi ametoa wito kwa waendesha vyombo vya moto kuheshimu sheria za usalama barabarazi na kutoa kipao mbele kwa wanafunzi pindi wanapo kuvuka barabara huku akisisitiza wananchi wanao ishi karibu na maeneo ya shule kuwa wazalendo kwa kuwasaidia wanafunzi kuwavusha barabara.

Kwa upande wake Elias makasi pamoja uongozi wa shule hiyo wamelishukuru Jeshi la Polisi Kwa kutambua mchango wao na kutoa elimu pamoja askari wa Usalama barabarani watakao shirikiana kuwasaidia watoto kuwavusha katika eneo hilo la Ihumwa kutokana njia hiyo kuu kuwa na wingi wa vyombo vya Usafiri.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea na mkakati huo wa kuzifikia shule zote zilipo Jijini Dodoma makundi mbalimbali ya watu ili kudhibiti ajali za Barabarani.








By Mpekuzi

Post a Comment

Previous Post Next Post