Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo akikabidhi vifaa vya TEHAMA kwa shule ya Sekondari Kishapu.
Na Sumai Salum - Kishapu
Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo ametoa vifaa vya TEHAMA vyenye thamani zaidi ya Tsh. Milioni nne kwa shule ya Sekondari Kishapu.
Akizungumza Leo Machi 22,2025 wakati akikabidhi vifaa hivyo katika viwanja vya shule kwa uongozi amesema ametimiza ahadi aliyowaahidi hivi karibuni ili kuboresha miundombinu kwa wanafunzi na walimu ili kuinua zaidi elimu.
Mhe. Butondo amesema msingi wa maisha ni elimu na Rais Samia Suluhu amekuwa akitoa fedha nyingi katika sekta ya elimu wakiwa ni mashahidi huku miundombinu ikiendelea kuboreshwa zaidi lengo likiwa kila mwananchi apate elimu bora.
"Vifaa ninavyotoa ni pamoja printa 1,projekta 1, power supply 5,computer screen 4,system unit 4 na televisheni 1, tafadhari naomba mvitunze sana ili na wadogo zenu wakija hapa wavikute ma viwasaidie kimasomo", amesema.
"Vifaa hivi vitumieni vizuri ili vidumu vikiwahudumia kwani Waalimu mtaandaa, kuchapa na kuzalisha mitihani kwa usiri hamtaenda mitaani kutafuta huduma hiyo itawapunguzia gharama na pia wanafunzi hawatakuwa na gharama kwenye kuzalisha masomo",ameongeza Mbunge huyo.
Akijibu taarifa iliyosomwa na mkuu wa Shule hiyo Madam Buhoro Mipawa iliyobainisha upungufu wa Madawati na viti vya wanafunzi 62, nyumba za kuishi waalimu 21,matundu ya vyoo 8, viti na meza 14 za walimu Butondo amesema atayawasilisha bungeni na mengine atayashughulikia.
Pia ametoa mchele zaidi ya kilo 150, mbuzi 5 pamoja na soda kwa wanafunzi wote wa Bweni kufurahia chakula cha jioni ikiwa ni moja ya hitaji lao walilomuomba.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe.Peter Masindi, Afisa Tawala Fadhiri Mvanga amempongeza Mbunge huyo na kuomba aendelee kusaidia na shule zingine huku akihimiza vifaa hivyo vitumike kwa lengo la kujifunzia pekee.
Naye Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Benard Werema amesema kitendo hicho kiwe funzo kwa watu wengine wenye nia ya kujenga Kishapu kusaidia mahali penye uhitaji shuleni.
Diwani wa Kata ya Kishapu Mhe. Joel Ndettoson amepongeza kitendo kilichofanyika kwenye Kata yake na amesema wanahitajika watu zaidi ili kusaidia jamii hiyo kwa lengo la kuwa wamoja.
Mwenyekiti wa Bodi ya shule Isack Masingija amempongeza Mbunge Butondo kwa moyo wa upendo na kuwathamini wanafunzi hao ambao wanatokea maeneo mbalimbali ya Tanzania huku akibainisha uwepo na changamoto ya uzio shuleni hapo hivyo pindi watakapohitaji msaada wake awasaidie.
Baadhi ya wanafunzi wameonesha kufurahishwa na kitendo hicho huku wakiahidi kuendelea kusoma kwa bidio zaidi kwani vifaa vya TEHAMA vitawasaidia katika kujifunzia.
Shule ya Sekondari Kishapu ilianzishwa mwaka 2004 na mwaka 2014 kupewa hadhi ya kuwa na kidato cha 5 na 6 inajumla ya wanafunzi 962 na waalimu 24 huku ufaulu wa kidato cha nne kuanzia 2022 hakukuwa na waliopata 0 huku kidato cha sita wakiwa ufaulu ukiwa ni daraja la 1,2 na 3 pekee.
Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo akizungumza na wanafunzi,waalimu,bodi ya shule ya sekondari Kishapu pamoja na kamati ya siasa ya kata ya Kishapu wakati akikabidhi vifaa vya TEHAMA vyenye thamani zaidi ya Tsh Mil.4 katika shule ya sekondari Kishapu.
Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo akizungumza na wanafunzi,walimu,bodi ya shule ya sekondari Kishapu pamoja na kamati ya siasa ya kata ya Kishapu wakati akikabidhi vifaa vya TEHAMA vyenye thamani zaidi ya Tsh Mil.4 katika shule ya sekondari Kishapu
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Kishapu Isack Masingija akizungumza mbele ya Mbunge Boniphace Butondo wakati akikabidhi vifaa vya TEHAMA shuleni hapo machi 22,2025
Mwanafunzi wa kidato cha tano shule ya sekondari Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Joseph Masasi akizungumzia umuhimu wa vifaa vya TEHAMA kwenye masomo yake.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Fadhili Mvanga akizungumza
Mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Suzan Jiyenze akielezea alivyofurahishwa na uwepo wa televishen shuleni hapo kwani itawasaidia kujua ulimwengu unavyoendelea
Diwani wa Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Joel Ndettoson akielezea kufurahishwa na tukio lililofanyika la utoaji vifaa vya TEHAMA shule ya Sekondari Kishapu kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo huku akiahidi kuwalipia kifurushi cha Televisheni kila kikiisha
Mmoja wa Skauti wa shule ya sekondari Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga wakimvisha skafu baada ya kumpokea shujaa wao Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Boniphace Butondo alipoenda kukabidhi vifaa vya TEHAMA vyenye thamani ya zaidi ya Tsh.MIL.4,Televisheni,mbuzi 5, mchele na vinywaji.
Mkuu wa shule ya sekondari Kishapu wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Buhoro Mipawa akisoma taarifa ya shule hiyo mbele ya Mbunge wa jimbo la Kishapu Mhe.Boniphace Butondo Leo Machi 22,2025 alipokuwa akikabidhi vifaa vya TEHAMA na vitu vingine.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Benard Werema
By Mpekuzi
Post a Comment