MWENYEKITI UVCCM KAGERA AMPAMBANIA RAIS SAMIA |Shamteeblog.



Na Lydia Lugakila - Karagwe 

Mwenyekiti wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UVCCM)Mkoa wa Kagera Faris Buruhan amewahimiza vijana Mkoani Kagera kutafuta kura za Mgombea Urais mwaka 2025 Dkt. Samia Suluhu Hassan ili Mkoa wa Kagera uweze kuongoza katika kura za jumla.  

Akizungumza na baadhi ya vijana katika Ukumbi wa CCM Uliopo Mjini Kayanga Wilayani Karagwe ikiwa ni Ufunguzi Wa ziara ya Siku kumi na sita ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM (UVCCM)Mkoa wa Kagera siku ambayo itakuwa maalum kwa kukutana na Vijana Wa Chama cha Mapinduzi CCM Faris amesema kuwa Vijana wa chama cha Mapinduzi wanatakiwa kutafuta kura nyingi za Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na Mgombea Urais kwa mwaka huu wa 2025 kwani tayari amepitishwa na wajumbe wa Halmashauri mkuu Kuwa Mgombea Urais . 

"Tunatamani sana Mkoa wetu upate heshima ya kuongoza kwenye kura za Dkt. Samia Suluhu Hassan lakini kura nyinyi kama Wanakaragwe wekeni malengo ya kusema kura za nchi nzima  au za Majimbo Karagwe iwe ya kwanza katika Kupiga Kura za Rais Samia”,amesema Faris.

Aidha Faris amewapongeza Wananchi wa Jimbo la Karagwe kwa Kuendelea Kumuamini Mbunge Wa Jimbo la Karagwe Mhe. Innocent Bashungwa ambaye ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi kwa kuwa Mbunge wao ambaye pia amewapatia fursa ya kuwatafutia miradi mikubwa ya Maendeleo ikiwemo miradi ya maji,afya na barabara.

Hata hivyo ziara hiyo itaendeshwa na kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Kagera, chini ya Mwenyekiti wake Faris Buruhani kwa siku 16 ndani ya Mkoa wa Kagera na Kampeni hii itapita kwenye wilaya zote 8 za Chama kwa  kuyafikia makundi ya Vijana wa Vyuo na Vyuo vikuu kwenye wilaya zote,Vijana wa Shule za Sekondari,Vijana waliopo vijiweni na mitaani,Vijana walioko kwenye kambi ya mafunzo,Vijana waliyojiajiri kwenye sekta zisizo rasmi,Viongozi wa dini na viongozi wa Kimila.









By Mpekuzi

Post a Comment

Previous Post Next Post