TAIFA GESI , UMOJA WA MAMA LISHE TANZANIA WAUNGA MKONO NISHATI SAFI YA DKT. SAMIA |Shamteeblog.


Baadhi ya akina mama wa Umoja wa Mama Lishe Tanzania (UMALITA) kulia wakipika futari kwa kutumia majiko ya gesi wakati wa hafla ya kusoma dua ya kumuombea Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania , Dkt. Samia Suluhu Hassan na watoto yatima wakati wa futari iliyoandaliwa na umoja huo kwenye viwanja vya mwembeyanga jijini Dar es salaam kwa udhamini wa Taifa gesi
Baadhi ya viongozi na wanachama wa Umoja wa Mama Lishe Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na Afisa Masoko wa Taifa Gesi, Anthony Martin kwenye shughuli ya kumuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na futari kwa ajili ya watoto yatima
Baadhi ya viongozi na wanachama wa Umoja wa Mama Lishe Tanzania wamekusanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusoma dua ya kumwombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwafuturisha watoto wa yatima ikiwa ni sehemu ya sadaka kwenye mwezi huu mtukufu wa Ramadhani


***
Umoja wa Mama Lishe Tanzania (UMALITA) umesoma dua ya kumwombea Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kumpongeza katika juhudi zake za kuhamasisha watanzania na matumizi ni nishati safi kwa ajili ya kupikia ili kuokoa mazingira.


Akizungumza jana kwenye viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Umoja huo , Jane Nyanda amesema kwamba umoja huo unaunga mkono kampeni ya Rais Dkt Samia Suluhu ya kampeni ya nishati safi.


“Tumekusanyika hapa kwa mambo mawili kwa ajili ya kumwombea Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake hizo za kampeni ya nishati safi kwa sababu sie mama lishe kampeni hii inatugusa moja kwa moja kwenye shughuli zetu za kila siku,”


“ukizingatia sisi ni mama lishe tunapaswa kuzungumza suala la nishati safi ili kuendelea kulinda mazingira lakini pamoja hayo pia tunaipongeza kampuni ya Taifa gesi kwa kutuunga mkono kwenye shughuli yetu hii,” amesema Bi. Nyanda


Amesema kampuni ya nishati ya Taifa gesi ni wadau wakubwa wa mama lsihe Tanzania na kampuni hiyo pia ni wawezeshaji wakubwa katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi hapa nchini.


Bi.Nyanda ameongeza kwamba mitungi ya Taifa gesi ni mizuri kwa ubora, ufungaji na ujazo wa gesi na ni salama kwa matumizi ya nyumbani , kwenye sehemu ya biashara na makazini.


Amefafanua kwamba shughuli hiyo ya dua ilikwenda sambamba na kuwafuturisha watoto yatima kwa kupikia mitungi ya Taifa gesi na njia moja wapo ya kuhamasisha watanzania waendelee kutumia nishati safi hata kwenye vituo ya watoto yatima.


By Mpekuzi

Post a Comment

Previous Post Next Post