Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe Boniphace Butondo na kamati ya siasa ya Kata ya Kishapu na Wialaya wakikabidhi jiko la gesi kwa Katibu wa BAKWATA Wilaya Ustadhi.Athman Ally Machi 22,2025 katika ofisi ya Mbunge
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe Boniphace Butondo, mwakilishi wa Mkuu 2a Wilaya na kamati ya siasa ya Kata ya Kishapu na Wialaya wakikabidhi jiko la gesi kwa Mwantum Salim Machi 22,2025 katika ofisi ya Mbunge
Na Sumai Salum - Kishapu
Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo amegawa majiko ya gesi kwa baadhi ya mamalishe,babalishe,watu wenye ualbino pamoja na nyumba za ibada.
Akizungumza wakati akikabidhi majiko hayo Machi 22,2025 kwenye ofisi ya mbunge amesema mkakati wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu ni kuhakikisha Watanzania wote wanaachana na matumizi ya nishati chafu ya mkaa na kuni na badala yake watumie nishati safi ya gesi na umeme.
"Kampeni hii imelenga kupambana na mabadiliko tabia nchi licha ya kukabiliwa pia na upungufu wa mvua lakini bado tunatakiwa tupande miti kwa wingi ili kurejesha uoto wa asili tulioupoteza baada ya kukata miti ili tupate kuni na mkaa kwa lengo la kupikia" ,amesema Butondo .
Aidha amesema ataendelea kuunga mkono jitihada za Rais kwa kuendelea kutoa msaada huo kwa nguvu zote kwani ukataji miti umepelekea ukame na hata kudidimiza Maendeleo ya jamii, taifa na viumbe hai vingine.
"Nimetimiza ahadi yangu mliyoniomba ya kuwapa majiko haya hivyo mkawe chachu ya mabadiliko kwa mamalishe wenzenu,baba lishe pia na nimetoa kwa Ostadhi kwani naamini anawafuasi wengi hivyo anaowajibu kuhakikisha elimu inatolewa kwenye nyumba za ibaada zote sio misikitini pekee" ,ameongeza Mbunge huyo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kishapu Peter Mashenji amesema jambo hilo ni sehemu ya utekelezaji ilani ya Chama hicho na wananchi wanapaswa kuitikia kampeni hiyo kwa vitendo.
Naye Diwani wa Kata ya Kishapu Mhe. Joel Ndettoson amemshukuru Mbunge na kusema ni neema kubwa kwa Kata hiyo ikiwa ni miongoni mwa Kata 29 zinazounda Wilaya kwani wajasiriamali watatekeleza shughuli zao vizuri huku mazingira yakibaki salama.
Baba lishe (muuza Kahawa na kuchoma chips) Masunga Kazi amepongeza kitendo hicho na kusema Mbunge hajabagua jinsia katika kutoa gesi na amegundua itamsaidia kuokoa muda kuliko matumizi ya mkaa ambapo alikuwa anatumia muda mwingi licha ya kuwa unagharama ambapo yeye kwa siku alikuwa akitumia debe mbili hadi tatu hivyo ukataji miti utapungua.
Mama lishe Neema Kisinza amesema kupata jiko la gesi litamsaidia kuondokana na adha ya kutumia muda mwingi kutafuta kuni kwa ajili ya kupikia kwani ni ghari na afya yake kuwa mashakani.
Jimbo la Kishapu lina jumla ya tarafa tatu Kishapu,Mondo na Negezi Mbunge ametoa zaidi ya majiko ya gesi 260 na ameahidi kuendelea kutoa ili kuepukana na matumizi ya nishati chafu yanayopelekea uharibifu wa mazingira hasa katika Wilaya hiyo yenye asili ya ukame.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe Boniphace Butondo akizungumza kabla ya kukabidhi majiko ya gesi kwa wajasiliamali na makundi maalumu kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita za kukabiliana na mabadiliko tabia nchi na kuachana na matumizi ya mkaa na kuni kupikia na kutimiza ahadi yake aliyowaahidi kwao Machi 22,2025 ofisini kwake.
Diwani wa Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Joel Ndettoson akizungumza kwa furaha baada ya Mbunge wa Jimbo hilo Mhe.Boniphace Butondo kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na kukabidhi majiko ya gesi kwa wajasiliamali na makundi maalumu Machi 22,2025 kwenye ofisi ya Mbunge
Mama lishe Neema Kisinza akizungumzia matumizi ya nishati safi kupewa jiko la gesi kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo Mhe.Boniphace Butondo Machi 22,2025 kwenye ofisi ya Mbunge yatakavyosaidia kumbadilisha kutoka matumizi ya kuni yanayopelekea kuhatarisha afya yake
Baba lishe Masunga Kazi akizungumzia umuhimu wa jiko la gesi alilopewa ba Mbunge wa jimbo hilo Mhe.Boniphace Butondo Machi 22,2025 kwenye ofisi ya Mbunge na kuondokana na matumizi ya mkaa huku akiokoa muda kwenye shughuli zake na kuongeza kipato huku mazingira yakiendelea kuwa salama
By Mpekuzi
Post a Comment